Shilingi bilioni 1.9 zimetengwa kwa mradi huo wa kutoa madawati kwa shule 15 za umma kwa kila kaunti ndogo chini ya mpango wa kufumua cuhumi kutumia madawati yanayotengezwa nchini .
Waziri wa elimu George Magoha amesema kwamba serikali imeweka mikakati ya kuzuia ufisadi katika mradi huo wakati alipokuwa akitoa mwongozo wa jinsi utakavyotekelezwa kwa makamishna wa kaunti .
“ Huu sio wakati wa kuuliza ‘mimi nitanufaika vipi’ huu mradi ni wa watoto wetu’ Magoha amesema
Waziri Magoha aliongeza kwamba shilingi bilioni1.9 zimetolewa chini ya mpango huo wa kufumua uchumi na unalenga biashara ndogo ndogo na za wastani .
Ili pawepo uwazi na kuepuka mapendeleo katika mradi huo serikali imetoa mwongozo utakaotumiwa ambao huwatambua wanaonufaika na fedha za kila wiki za walioathiriwa na Covid 19 .
Katibu wa kudumu wa usalama wa ndani Karanja Kibicho amesema ana matumaini kwamba maafisa wa utawala na serikali wataonyesha uadilifu katika usimamizi wa mradi huo .
Mradi huo utapelekea madawati 622,367 na viti yanatolewa kwa shule za umma huku serikali ikiendelea kuweka mikakati kwa matayarisho ya kufunguliwa kwa shule .