monicah-kimani1

Maisha ya raha mstarehe aliyoishi Monica Kimani

Wakenya wamepata jipya la kuangazia kutoka kwenye kesi ya mauaji yake Monica Kimani.

Monica alikuwa mfanyi biashara maarufu hapa nchini. Alipatana na mauti yake nyumbani kwake eneo la Lamuria Gardens. Monica alitambulikana sana kwa maisha yake ya kistaarabu pamoja na kuendesha magari makubwa ya kifahari.

Afisa wa polisi aliyefika eneo hilo mapema, Jennifer Sirwa alitoa picha za sehemu ya shingo ya marehemu Monica. Mdomoni alikua amefungwa na kamba nyeusi huku miguu ikifunganishwa nyuma nayo mikono ikafungwa nyuma.

Moja kati ya picha zilizotolewa zilimwonesha monica akiwa kwenye bafu huku amevalia vazi refu ya kijani kibichi, miguu yake ikiwa imeinuliwa juu na mkato wa sentimita sita kwenye shingo lake.

Kwenye mkono wake uliojaa michoro mlikua na huku kamba za kushindilia  paa la nyumba. Sirwa alidai kuwa Monica aliuliwa sebuleni mwake kisha mwili wake ukavurutwa hadi bafuni.

“Mlikua na taulo iliyolowa damu ambayo tunashuku ilitumika kuosha damu kutoka sebuleni.” Alieleza Sirwa.

Hata hivyo wakili wake Joseph Irungu,Hassan Nandwa, alidai kuwa huenda Monica aliaga dunia kutokana na njaa kwani uchunguzi wa mwili ulionesha ukosefu wa chakulab mwilini mwake.

“Je, mlifugua umio wake ili kubaini alichkuwa kale hio siku? Je, mlifumgua tumbo lake? Je, twaweza kusema kuw kifo chake ni sababu ya kukosa kula kwani hamkua na chakula tumboni mwake?

Monica KimaniMonicah Kimani
Marehemu Monica Kimani

Wakili Hassan pia alikuwa amedai kuwa labda shingo lake monica ilikatika baada ya kupiga dunia teke.

Ndegwa alisema,”Mwili ulikua unatoa damu. Hakuna mwili mfu hutoao damu. Alikuwa na mkato kwenye shingo lake ulionekana  na damu iliyojaa kwenye mapua.”  Uchunguzi wa mwili ulifanyika tarehe 24 kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo. kulinganan na uchunguzi ,monica aliaga dunia kutokana na kidonda cha kitu chenye makali. viuno vyake vyote vilikuwa na vimefungwa na kanda nyeusi.

“Mwili huo ulikuwa wa mtu mwenye umri wa miaka 28, alikuwa kavaa nguo ya rangi ya samawati  na alikuwa na vazi refu la kijani kibichi,” Ndegwa alisema. kulikuwa na wakati ambapo jaji aliuliza,”Je, mlikuwa mnaitazama kana ya soap  ama cinema ya Nigeria? Hii ni baada ya daktari wakufanya uchunguzi wa wafu kuleta picha nyingine..

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments