Maisha yangu yamo hatarini, Asema Waiguru

Picha: Businessdaily

Aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru amesema maisha yake yamo hatarini na anawataka polisi kumpa ulinzi zaidi.

Waiguru ameamwandikia barua inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett akitaka kupewa ulinzi kwani ametishwa na watu mashuhuri akiwemo kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale kufuatia hati yake ya kiapo iliyowataja baadhi ya viongozi waliohusika na sakata ya NYS.