Majaribio ya kuinua upendo wafika hadi mahakamani

Wazungu walisema upendo ni kipofu lakini upendo ni kila kitu? Na kweli upendo ni kipofu kweli?

Vazi la ndani la wanawake yaani sindiria limetengenezwa ili waweze kujiamini zaidi. Lakini limemuingiza msichana mnyenyekevu Eveline Kemutu katika shida nyingi.

Eveline alipata kazi katika mtaa wa Kariobangi South kaunti ya Nairobi. Mkataba wake hukusimamishwa tu lakini  amepatwa na kesi kortini.

Siku moja tu mwezi wa Januari mwajiri wake Lydia Atieno, alikuwa  anachekewa kuenda kazini, kwa maana hakuwa anapata sindiria yake.

Aliamua kumuuliza mfanyakazi wake Kemutu, kama aliweza kuona sindiria yake, tuhuma zake Atieno zilimwezesha kuenda kuangalia mfuko wake Kemutu.

                                                     Majaribio ya kuinua upendo wafika hadi mahakamani

Aliweza kumpata Kemutu amevaa sindiria yake. Si sindiria tu pekee aliweza kupata sufuria zake za shillingi 25,000 ziliwa zimefichwa chini ya kitanda ya Kemutu.

Zaidi ya yenye alikuwa amefanya, si kwa muda mrefu lakini Kemutu alijipata mahali pabaya yaani alijipata akiwa korokoroni.

Jana Eveline alililambia korti ya makadara kuwa ilikuwa makosa ya utambulisho.

Kemutu alieleza korti kuwa alinunua sindiria hizo sawa na za mwajiri wake Atieno, hii bi baada ya mpenzi wake kutorithika na sindiria za awali alizokuwa nazo kisha akaenda kununua sindiria sawa na za Atieno.

Mwanamke huyo mwenye dhiki alisema hakuiba sindiria hiyo bali alinunua na pesa zake. Mwenyewe alieleza hayo mbele ya hakimu mkuu wa korti ya makadara, Eunice Opondo.

"Mheshimiwa nilinunua sindiria hizi na pesa zangu mwenyewe sikuiba,ni vile zina fanana na za mwajiriwa wangu,"Alisema Kemutu.

Kufuatia kisa ambacho amekumbana nacho, Kemutu hajui aache kupenda ama aendelee tu na kupenda mwanaume ambaye anataka mapenzi ya hali ya juu.

Nikitia kikoma upendo wa sindiria umeweza kumfanya Kemutu kupatwa na mashtaka ya kuiba sindiria isiyozidi shillingi 500.

Huku akiachiliwa na dhamana ya shillingi 50,000 na kesi kusikizwa Aprili 8. Vazi ndogo lililomuingiza Eveline Kemutu mashakani.