Makasisi wapinga ndoa za jinsia moja

Picha kwa hisani ya: usnews.com

Serikali ya kitaifa imeombwa kuzidisha juhudi zake katika vita dhidi ya ufisadi nchini ikizingatiwa kuwa ndicho chanzo kikubwa cha umaskini. Haya ni kwa mujibu wa viongozi wa madhehebu nchini (NCCK) katika eneo la magharibi.

Makasisi hao wakiongozwa na Daktari Nelson Makanda wamedai ufisadi ni kama janga linalolemaza uchumi wa taifa hili.

Vilevile makasisi hao wamepinga vikali ndoa za jinsia moja huku wakisema kuwa kama kanisa hawakubaliani kabisa na kuwa uamuzi wa mahakama haukuwafurahisha na kuongeza kuwa watafuata neno lililo kwenye bibilia.

Aidha walipinga vikali suala la serikali kunyakua mashamba yaliyojengewa shule na makanisa na kuzifanya shule hizo kuwa za umma chini ya serikali.