Mama atafuta haki ya mtoto aliyebakwa

Maisha ya mwanamke mmoja kwa jina Caroline Akeyo yamo hatarini kufuatia juhudi zake za kumtafutia haki bintiye anayedaiwa kubakwa na

shemejiye.

Akiongea na wanahabari Caroline Akeyo alisema kuwa mshukiwa huyo anadaiwa kumbaka mwanawe wa miaka kumi na mbili akitoka kanisani

wakati mamake alipokuwa safarini na aliporudi akaelezwa na mama huyo.

Mwanamke huyo aliripoti kisa hicho kwa chifu wa eneo hilo John Agoro huku juhudi zake za kupata haki zikigonga mwamba.

Kulingana na OCPD wa Rongo Jonathan Kisaka Muganda,familia ya mshukiwa huyo ilikuwa tayari imefanya kikao cha kutatua jambo hilo bila ya

kumhusisha mamake mtoto huyo jambo ambalo lilimghadhabisha zaidi na kuripoti kwa polisi.