Mambo 3 wanawake hufanya ambayo hukasirisha wanaume kabla ya 'Twa twa'

twa
twa
Mara kwa mara kuna mambo ambayo wanawake hufanya ambayo humaliza kabisa ile hamu ya kushiriki mapenzi na wapenzi wao.

Hata hivyo, kama wanaume, sio kila wakati tutaketi chini na tuwaeleze au kuwafahamisha wake au wapenzi wetu kuhusu makosa hayo.

Tumeorodhesha mambo kadhaa ambayo wanawake hufanya kabla ya kushiriki Twa Twa, ambayo kwa kweli huvunja hamu ya wanaume kitandani.

  1. Kuzungumzia mpenzi wako wa zamani

Kwa hakika ni nani aliye na akili timamu ataketi kando yako na kuskiza kuhusu jinsi mpenzi wako wa zamani alikuwa anakufanyia wakati wa ngono? Ebu tafakari akikusimulia jinsi alivyopenda akimgusa au akimdekeza. Jameni!

2. Kujitandaza kitandani kiholela

Kabla ya twa twa, kuna mambo kadhaa unayopaswa kufanya au kumfanyia mumeo. Kwa mfano unaweza kumlaza chini na kumkanda mwili, labda umpake mafuta yenye manukato badala ya kujitandaza kama maiti ukimngoja aanze safari ya Mombasa raha.

3. Kuvaa mavazi kama gunia

Yaani una nia moja tu ambayo ni kumpa mumeo au mpenzi wako hamu ya kukupa mahanjam usiku mzima, lakini badala ya kuvalia suruali fupi, rinda rembo unavaa shati ya Safaricom. Utalala pekee yako.