File photo dated 13-08-2016 of Manchester City manager Pep Guardiola, who was satisfied with what he called "the first step" after launching his Manchester City reign with a victory. PRESS ASSOCIATION Photo. Issue date: Sunday August 14, 2016. See PA story SOCCER Man City. Photo credit should read Anthony Devlin/PA Wire.

Man City watanipiga kalamu nikishindwa kuwanyuka Madrid – Guardiola

Pep Guardiola amedai kwamba Manchester City huenda ikamfuta kazi iwapo watashindwa kuilaza Real Madrid katika kombe la mabingwa Ulaya. (Guardian)

Hatahivyo kufutwa kazi kwa Guradiola sio kitu rahisi kutokana na rekodi yake bora alioiweka baada ya kushinda mataji matano muhimu licha ya kushindwa kuiepeleka mbele ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa katika majaribio matatu.

Arsenal vs Man City: Baada ya kupokea kichapo dhidi ya Man United, Guardiola ataandikisha ushindi leo?

Manchester United imeruhusiwa kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23, kwa dau la £60m deal. (Star)

Chelsea pia imepatiwa motisha wa kumsaka Dembele huku rais wa Lyon Jean-Michel Aulas akikiri watamuuza mchezaji anayetaka kuondoka “. (Mail)

Tottenham inafikiria kumsaini beki wa Norwich na England mwenye thamani £50m Ben Godfrey, 22. (Express)

Paris St-Germain imejianda kumpatia mshambuliaji wake Kylian Mbappe kandarasi ya malipo ya £41m kila mwaka ili kuzuia kumpoteza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwenda Real Madrid 2021. (Mirror)

Guardiola athibitisha kuwa atakosa huduma za mshambulizi Sergio Aguero

PSG ina mpango wa kumsaini kipa wa Man United mwenye umri wa miaka 22 Dean Henderson, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United. (Mail)

Kylian Mbappe

Aliyekuwa beki wa England Joleon Lescott amemuonya kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, kutojiunga na Manchester United mwisho wa msimu huu kwa kuwa huenda wasifuzu kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.. (Standard)

Real Madrid iko tayari kuilipa Inter Milan £120m zinazohitajika kumuachilia mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka katika kandarasi (TyC Sports)

Tottenham inapanga kumsherehekea mfungaji wa magoli mengi zaidi katika klabu hiyo ambaye amefikisha umri wa miaka 80 Jimmy Greaves kabla ya mechi yake ya ligi ya mabingwa kati yake RB Leipzig wiki ijayo. (Standard)

-BBC

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments