Maraga kuunda jopo kusikiliza kesi yake Omtatah

Jaji Weldon Korir amelitaja kesi iliyowasilishwa na mtetezi wa haki za kibinadamu Okiya Omtatah kuwa na uzito mkubwa.

Korir ameongeza na kusema kuwa maswala yaliyotajwa mle ndani yanaibua maswali muhimu ya kisheria.

Jaji huyu ametuma ombi kwa  jaji mkuu David Maraga kuunda jopo la majaji litakalosikiliza kesi hiyo.

Soma hapa:

Okiya Omtata mapema jana alifika mahamakani kupinga swala la kuidhinisha noti mpya zitakazotumika nchini kuanzia tarehe 1 Oktoba. Katika stakabadhi alizowasilisha mbele ya mahakama, Okiya anahoji kuwa ni ukiukaji wa sheria katika mpya ya 2010 kuchapisha hela iliyo na picha ya muasisi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

Mwingine aliyefika mahakamani ni mbunge wa EALA Simon Mbugua mapema jumatatu ili kukataa katakata uidhinishwaji wa noti mpya. Mashtaka ya Simon dhidi ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) yanaendana sawa na yake Okiya Omtatah.

Soma hadithi nyingine hapa:

Gavana wa CBK, Patrick Njoroge katika kikao na wanahabari alisema kuwa yupo tayari kukabiliana na mashtaka yoyote mahakamani. Njoroge alisema kuwa sheria imefuatwa katika mchakato huo na kwamba lengo kuu ni kuzima moto wa ufisadi na wizi wa pesa nchini.

Noti za awali za elfu moja zitapigwa marufuku na kuacha kutumika tarehe mosi Oktoba. Wananchi wanaombwa kubadilisha noti mzee katika tawi la benki iliyo karibu kabla ya muda huo kufika.

Mengine yanafuata…