Masaibu ya Monroe! Akubali kuwa mraibu wa Marijuana

103884270_255347392409512_6597211989333038278_n
103884270_255347392409512_6597211989333038278_n
Mfanyabiashara maarufu wa Twa Twa nchini Huddah Monroe amethibitisha kuwa ni shabiki sugu wa marijuana kutoka enzi za kitambo.

Huddah amesema kuwa kutokana na ukwasi wa mihela alionao anaweza kununua kila aina ya chakula, magari, vinywaji na vingine ili kusherehekea kujituma kwake katika biashara hiyo.

Jumanne Huddah aliwatunuku muda wa kipekee mashabiki wake kumuuliza maswali kuhusiana na yale mambo wasiyofahamu kumhusu.

Bila ya kupoteza muda, kichuna huyo alirekodi video akiwa anajivinjari na Marijuana ili kuwafahamisha wafuasi wake kuwa amekuwa akishabikia matumizi yake kwa muda.

; ‘’Cigarillo life. City of lights lights,’’alifuatisha ujumbe huo.

Kwa muda kichuna huyo hajawahi kuwafichulia watu kuwa anapenda marijuana japo video hiyo sasa iliweka mambo mubashara.