Mastaa wa mziki waliofariki kabla ya nyota zao kung'aa zaidi

Kenya imekuwa na wanamziki wengi ambao walitoa  upya mziki wa nchi hii lakini kabla ya hata nyota zao kung'aa zaidi kifo kikawachukua.
Hata hivyo  nyimbo za baadhi yao zingali  zinavuma na kumbukukumbu na kazi zao zaendelea kuonekana.

 

Sagini

Mwaka uliopita mwezi Disemba tulimpoteza mwanamziki chipukizi  Sagini baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Alifariki baada ya kuuga kwa muda mfupi alipolalamikia maumivu  wakati  wa  mahojiano kwa runinga katika stesheni    ya NTV. Baada ya hapo alipelekwa hospitalini na aliaga dunia muda mfupi baadaye.

Sagini alikuwa amejisajili na kampuni ya mwanamziki maarufu Khaligraph Jones BluInk Corp na alitoa wimbo naye uliovuma sana unaojulikana kama Testimony.  Alifariki mwezi Disemba tarehe 17 mwaka 2018.

Kaberere 

Mwanamuziki  huyo mashuhuri wa nyimbo za injili alifariki Aprili tarehe 6 mwaka 2014 . Alifariki baada ya kupigwa na umeme akiwa katika duka lake la kuosha magari.

Kaberere alivuma sana baada ya kibao chake "Kiburi ni cha nini?'' 

Aliwaacha mke ambaye alikuwa mjamzito wakati huo na mtoto mmoja wa kiume.

Angela Chibalonza

Angela Chibalonza  alikuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili  na alifariki tarehe 22 mwezi September mwaka 2007  baada ya kuhusika katika ajali ya barabara katika eneo la Kinale  kwenye barabara ya Naivasha -Nairobi.

Angela alijulikana kwa vibao vyake vilivyovuma mno kama vile Ebenezer, Kaa nami, Tamu na vingine. Alimwacha mume na mtoto mmoja wa Kike.

Nyimbo zake bado zinavuma miaka kumi na mbili baadaye.

E-sri

Issah Mmari Wangui,  alikuwa msanii wa nyimbo za kufoka aliyejulikana kwa jina lake la kisanii E-Sir alifariki mwaka 2003 mwezi Machi tarehe 16 baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani.

Hata baada ya miaka 16 ya kufa kwake bado anachukuliwa kama mmoja  wa wasanii bora aliyewahi kuwepo humu nchini.

Anajulikana kwa nyimbo kama vile Boomba Train, Hamnitishi, Moss Moss na Kamata miongoni mwa nyingine.

 Krupt 

Carlton Williams Bongo Juma almaarufu K-rupt alikuwa  mwanamziki wa nyimbo za kufoka vilevile ambaye alikuwa na umaarufu wa kimataifa katika miaka yake miwili ya usanii kabla ya kuuawa mwaka 2003. Alifanya muziki na wasanii kadhaa kama vile Fizzle Dogg, Bigpin na E-sir.

Lady S

Kila mwaka mashabiki, jamaa na marafiki hukongamana ili kumkumbuka malaika wa Calif Lady S na maisha yake.

Lady S, mwanamziki wa nyimbo za kufoka alifariki September mwaka 2007 na anakumbukwa  kamo mmoja wa wanawake ambao waliweza kurekodi nyimbo na Clemmo.

Alirekodi nyimbo na Pilipili na vilevile alikuwa katika kundi la wasichana pekee la Calif Angels pamoja na Choku na Ratatat.

Lady S alifariki katika ajali ya barabara.