Matiang'i aagiza kurejeshwa makwao Wachina wanaofanya biashara Gikomba

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi  ameagiza kurejeshwa nchini mwao raia wa Uchina  wanaofanya biashara  katika soko la Gikomba  hapa jijini . Matiangi amesema wachina hao wapo nchini kinyume cha sheria . Matiangi amesema raia wote wa kigeni wanaoshiriki biashara ndogo ndogo nchini watarejeshwa makwao.

Matiangi  amesema  serikali haziwei kuwapa  vibali raia wa kigeni kufanya kazi  ambazo wakenya wanaweza kuzitekeleza . ‘Nimeziagiza idara za usalama kuhakikisha kwamba wale wanaofanya biashara Gikomba ,wanarejeshwa makwa’ amesema waziri Matiangi akiwa Nakuru wakati wa ufunguzi wa afisi ya kushughulikia paspoti .

Amesema vibali vya kufanya kazi nchini vina masharti mugumu sana kwa raia yeyote wa kigeni na  masharti hayo yanafaa kutekelezwa ili pia kuzilinda biashara na maslahi ya wakenya .

Kumekuwa na lalama hasa katika mitandao ya kijamii baada ya gazeti mmoja nchini kuchapisha taarifa na picha za raia wa Uchina ambao wanauza nguo za mitumba katika soko la Gikomba .Wakenya pia hawajapendezwa na hatua ya wachina kuingilia biashara ndogo ndogo kama vile uchuuzi katika sehemu mbali mbaliz a taifa .