Matokeo ya KCSE: Idadi ya wanafunzi waliopata alama ya 'A' yaongezeka

maghoha
maghoha
Jumla ya wanafunzi 627 walijizolea alama ya 'A' katika  mtihani wa mwaka huu wa KCSE, kutoka 315 mwaka jana, waziri wa elimu George Magoha amesema.
Mwanafunzi bora ni Tony, kutoka Shule ya Upili ya Kapsabet ambaye alijizolea gredi ya A yenye alama 87.159.

Baraza wa shule ya upili ya Kenya High alijizolea gredi A yenye alama 87.087.

Kaboge Odhiambo kutoka shule ya upili ya Kapsabet alipata gredi A na alama 87.080, Antony Owuor alipata A ya alama 87; Natasha Wawira wa Kenya High alipata gredi ya A ya alama 86.9.

"Matokeo yanaonyesha uboreshaji mkubwa ukilinganisha na yaliyoshuhudiwa katika miaka mitatu. Walimu wetu wanawashirikisha watahiniwa bora. Kwa hivyo naweza kusema hakukuwa na wizi wa mtihani," Magoha alisema.

Wanafunzi waliopata alama ya A- walikuwa 5,796, ikilinganishwa na 3,318 mwaka uliopita.
Matokeo yalitangazwa siku tatu mapema kuliko ilivyokuwa mwaka jana.

Idadi ya watahiniwa 125, 746 walijizolea alama ya C+. 2018 idadi ya watahiniwa 96,377 ndio waliojizolea C+.

Jumla ya wanafunzi 699,745 walifanya mtihani wa KCSE mwaka huu ambao ulikamilika November 27.

Mwaka uliopita, Juliet Otieno kutoka shule ya upili ya Pangani ndiye aliyeongoza baada ya kujizolea alama 87.6, huku akifuatwa kwa karibu na Kaluna James wa chuo kikuu cha Maseno na alama 87.3.

Hata hivyo, 2018 watahiniwa wa kiume ndio waliotawala orodha ya watahiniwa 100 bora.