Mazoezi rahisi yanayoweza kuchonga kila sehemu ya mwili wako

Unatafuta njia za kupunguza uzani bila kwenda gym  kwa sababu ya shughuli za kikazi ,shule au umebanawa kabisa ?

Usiwe na wasi wasi kwani kuna mazoezi  mepesi  unayoweza kufanya ili kuafikia malengo yako ya kuthibiti uzani .

 Fanya mazoezi ya kurukaruka na kujishashua ‘ Aerobics’

Aerobics  ni aina ya mazoezi  yanayokuwezesha kuufanyisha moyo  harakati za kufanya kazi vyema  .unaweza kushiriki uogeleaji ,kutemebea ,kuendesha baiskeli na kadhalika .

Mazoezi hayo kwa jina cardio huweza kukusaidia kumaliza mafuta mwilini

Unaweza kuyapata mazoezi ya aerobics kupitia video za youtube  au katika warsha za mazoezi . huhitaji kwenda gym kwa hilo.

Planks

Haya ni mazoezi ya kufanya mwili thabiti .yanasaidia  kumaliza mafuta katika  sehemu ya tumbo .unaweza kuyafanya mazoezi haya baada ya kazi  au hata nyumbani  .utahitaji tu kuyashiriki kwa sekunde 30 kwa  seti mbili .kwa  mwezi mmoja tu utaanza kuona tofauti kubwa .

Jumping jacks

Haya ni mazoezi rahisi ya kuruka  ambayo unafaa kuyafanya ukibadilisha  kiwango cha nafasi kati ya miguu yako  huku mikono yako ikiwa juu . unayaweza kuyafanya mara 50 katika seti mbili  na utahisi  uwezo wake .

Kudensi

Kudensi ni mazoezi yanayohusisha mwili mzima na pia yanapendeza . ni mazoezi bora sana kwa moyo wako  na pia yanakusaidia kuainisha  voungo vya mwili .

Unaweza  kufanya mazoezi haya ni rafiki zako  au familia mnaposikiliza muziki  na pia kuchoma mafuta wakati huo huo . ni  jambo linalosajili faida  mara dufu .

Lunges

Lunges  ni mazoezi  yanayosaidia  kulainisha  muonekano  wa sehemu za chini za mwili ili kukupa nguvu zaidi . pia  yanakusaidia kuondoa  mistari  ya ufuta inayojiwamba kwenye ngozi    yaani  cellulite .

Unaweza kufanya seri 10 ya mazoezi haya kila siku  kwa mwezi mmoja ili kushuhudia matokeo .

Squats

Haya ni mazoezi ya sehemu za chini za  mwili  yanayolenga kuimarisha misuli  ya miguu , paja na sehemu ya nyuma .

Unaweza kuyafanya mazoezi haya popote wakati wowote .seti 25  kila siku  ni kiwango bora .