Ilikuwa ni ishara tosha kwamba rais mstaafu Marehemu Moi alikuwa amemchagua mwanawe wa mwisho wa kiume kuchukua usukani wa kuiongoza familia hiyo kisiasa . Watu waliofahamu mipango ya familia Ya Mzee Moi wamesema kabla hata ya hafla ya jana ya Gideon kukabidhiwa rungu hiyo na kakake Raymond ,Moi alikuwa ameshatangaza kabla ya kifo chake kwa Gideon Ndiye atakayemrithi kisiasa.
Kingpin? Gideon Moi apewa ‘rungu’ ya Mzee Moi na familia yake.
Kisha alianza kumfunza mambo ya kumwezesha kuchukua jukumu hilo na tangia hapo Gideon Moi alikuwa karibu sana na babake . Inafahamika kwamba Mzee Moi ndiye aliyemshinikiza mwanawe kujiunga na siasa na pia kukiongoa chama Cha KANU .
Kuidhinishwa kwa Gideon kama mrithi wa Mzee Moi sasa huenda kukafungua wamu nyingine kali ya malumabno ya uongozi wa jamii ya wakalenjin na naibu wa rais William Ruto . Gideon hakutarajiwa kulingana na mila za wakalenjin kuwaruka kakake zake wakubwa marehemu Jonathan na mtoto wa pili wa Mi Raymond ili kuchukua usukani wa kisiasa wa familia yake . Lakini uamuzi wa familia kubwa ya Chepkeres kumpa uongozi wa kisiasa wa familia huenda umethibitisha uamuzi wa marehemu Mzee Moi . Baada ya Gideon kupewa jukumu hilo ,hofu iliyokuwepo ya uwezekano wa kuzuka mgawanyiko sasa imefutiliwa mbali .