MBOCH PIA NI BINADAMU:‘Nilikuwa nikiosha chupi za mwajiri wangu na kutupa ‘pads’ zake’-Mfanyikazi wa nyumbani asimulia masaibu yake .

‘Mamboch pia ni binadamu  na ni watoto wa watu’. Hiyo ndio kauli ya kwanza inayotoka kinywani mwa  Sylvia Namuye ambaye amefanya kazi ya nyumba hapa Nairobi na katika sehemu nyingi za nchi kwa zaidi ya miaka 15 .

Silvya ,mwenye umri wa miaka 37 , ameamua kuzungumza kuhusu masaibu wanayopiotia wafanyikazi wa nyumbani hasa baada ya aliyelikuwa mfanyikazi wa mtangazaji  Betty Kyallo, Consolata Wawira  kujitokeza kufichua  mateso aliokuwa akipitia chini ya mwanahabari huyo .Consolata na Betty wamekuwa na majibizano ya mtandaoni lakini sasa ,Namuye anasimulia baadhi ya mateso na jinsi waajiri wengine hawana utu . Alipomaliza   darasa la nane kwao huko Butere,Namuye alichukuliwa na jamaa yake mmoja kwenda  Nakuru kumfanyia kazi ya kulinda mtoto.Hapo ndipo safari yake ya kufanya kazi za nyumbani ilipoanzia na amewafanyia zaidi ya watu watano kazi hiyo lakini masimulizi yake yanamlenga mwajiri wake mmoja mtaani  Loresho ambaye ukatili wake kamwe Namuye hataowahi kuusahau .

Sylvia anajua kazi yake vizuri na ratba hutolewa kwa kila mfanyikazi wa nyumbani.Lakini mateso aliopitia  chini ya familia moja iliyompa kazi loresho hayatowahi kufutika kutoka kumbukumbu zake . kando na mama mwenye nyumba kutojali,watoto wake watatu waliokuwa na umri wa kwenda shule hawakua na adabu hata kidogo na walikuwa wakimtolea maagizo kama mtoto alipokuwa akiwafanyia kazi . Kilichomshtua Sylvia ni baadhi ya vitu alivyohitaji kufanya  ingawa anasema alivumilia kwa sababu ya mshahara mzuri wa shilingi elfu 15 aliokuwa akilipwa . Mume wa mama mwenye nyumba alikuwa jamaa mpole na wakati mwingi alikuwa katika safari za kazi .Wakati wote hakujua mateso ambayo Sylvia alikuwa akiYApitia . Baadhi ya kazi alizotakiwa kufanya bila kupenda ni-

1.Kuosha Chupi ya mama mwenye nyumba

  Sylvia anasema kila mfanyikazi wa nyumbani anajua na anakubali kwamba kufua nguo ni sehemu ya kazi yake ,lakini mwajiri  wake alikuwa akimtolea chupi zake za hata wiki moja na kumtaka azifue .

‘SIJAWAHI KUDUNISHWA HIVI.MWANAMKE ALIYEKOMA NA CHUPI ZAKE KUBWA KUBWA ALINIWEKEA MRUNDIKO KIL WIKI KUZIFUA.HAKUWA MSAFI NA YOU CAN IMAGINE JINSI NILIVYOMANAGE KUZISAFISHA ZING’ARE’. Anasema Sylvia .

Ameongeza kwamba licha ya kujizatiti kadri ya uwezo wake ,wakati mwingine mama mwenye nyumba angemfokea kwa ukali akisema kwamba sylvIa hajaziosha vyema chupi zake ,na angefanya hivyo mbele ya watoto .

2.Kutupa ‘pads’ zilizotumika

  Kila mwanamke mwenye kwenda hedhi anajua kwamba ni  busara yeye mwenyewe  ajitupie vitambaa vyake vya  hedhi baada ya kuvitumia .Lakini mwajiri wa Loresho alikuwa akivitumia  visodo vyake na kuviacha kwenye  kipipa cha taka .Mfanyikazi wake wa nyumbani, Sylvia ndiye aliyeachiwa kazi ya vitupa .

 ‘ NILIPOANZA KUTUPA HIZO PADS NDIO NIKAJUA HII KAZI NITAIACHA .BUT NIKIKUMBUKA KUNA WATOTO WAWILI WANAONGOJA CHAKULA NYUMBANI,NILIVUMILIA TU’  anasema Sylvia

3. Ukatili na kukosa kujali

Kando na kazi ambazo hazifai kupewa mtu mwingine kufanya ,Sylvia anasema kuna vitu ambavyo mwajiri wake alikuwa akifanya na kusema ambavyo vilimfanya ajichukie . Walipokuwa wakitoka kwenda mkahawani kwa mfano ,anasema alikuwa akiachwa nje ya makahawa.Mama mwenye nyumba na mumewe na watoto wao wangekuwa ndani ya mkahawa wakila ,kisha mfanyikazi wao angeachwa   ndani ya  gari nje ya mkahawa . Nyumbani ,ilikuwa sheria kwamba Sylvia hangeweza kulala kabla ya watu wote wa familia kuingia katika vyumba vyao kulala .Ilikuwa sheria ambayo hangeweza kuikaidi hata awe mchovu namna gani . Kilichomfikisha mwisho Sylvia hata hivyo ni  hatua ya mama mwenye nyumba kukosa utu wa kumruhusu apate likizo ya kupata matibabu alipokuwa mgonjwa .

‘ Siku moja nimepatwa na Tonsils,wiki yote nilijikaza kufanya kazi bila hata kupumzika lakini mwajiri hakusema lolote!’ Alipochukua likizo ya disemba mwaka wa 2019, Sylvia hakurejea kwa mwajiri wake Loresho .