Wajir Woman Representative Fatuma Gedi during a press briefing in which she denied bribing MPs to shoot down the sugar report in August 13, 2018. /JACK OWUOR

Mbunge wa Wajir Mashariki  Rashid Amin amshambulia  Mwakilishi wa akina Mama  Gedi

  Mbunge wa wajir mashariki Rashid  Amin ameshtumiwa kwa kumshambulia mwakilishi wa akina mama wa wajir   Fatuma Gedi katika majengo ya bunge mapema alhamisi .  kisa hicho kilifanyika katika eneo la kuegesha magari bungeni  wakati Bi.Gedi alipokuwa na  mwakilishi wa akina mama wa homabay  Gladys Wanga  walipokuwa wakielekea mkutanoni aliposhambuliwa na Bwana  Amin .

Bwana Amin alimshtumu Bi Gedi ambaye ni mwanachama wa kamati ya bajeti kwa kukosa kulitengea eneo bunge lake pesa  wakati wa ziara ya hivi karibuni ya kamati hiyo katika kaunti ya Wajir .

Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 13 Juni 2019

Baada ya dakika chache Bw .Amin alimpiga  Bi.Gedi ngumi usoni  na kumwacha akivuja damu   huku Amin akizuiwa na mbunge wa Wajir magharibi  Ahmed Kolosh . Bi.Wanga aliyeshuhudia tukio hilo  amesema walikuwa pamoja na Gedi wakati alipoviziwa na  Bw. Amin . Gedi alikimbizwa katika hospitali ya Karen  kwa matibabu na baadaye akahudumiwa na  daktari mmoja wa polisi . Suala hilo limeripotiwa katika Kituo cha polisi cha bunge  kama OB/20/13/6/2019.

 

Kauli Ya siku 13th June 2019

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments