Mcheshi Churchill azungumzia azma yake ya kustaafu

churchill-compressed
churchill-compressed
Mwigizaji  na mcheshi Daniel Ndambuki almaarufu Churchill amezungumzia kuhusu kustaafu kwake.

Ijapokuwa amekuwa mcheshi maarufu sana kwa kipindi cha mwongo moja, kuna mengi usiyoyajua kumhusu nyota huyu.

Akihojiwa na World Is Jumatano, Churchill alisema kuwa alifahamu fika kuwa hatasalia katika fani hiyo maisha yake yote na hiyo ndio sababu kuiweka familia yake faraghani.

"Baada ya kuhudumu machoni pa umma jinsi nimekuwa kwa muda huo wote, wakati utafika ambapo  nitaishi maisha yangu faraghani pamoja na wale ambao wamekuwa wakinipa motisha," alisema.

Churchill alisisitiza kwamba watu mashuhuri wanafaa kuziweka familia zao mbali na umma ili waweze kutimiza malengo yao maishani.

Mcheshi huyu ameimarisha vipaji vingi sana vya wacheshi wanaoibuka.

Soma taarifa nyingine:

Alisema kwamba marehemu babake alimfunza kuwa na adabu na kuwa mchapa kazi mwaminifu.

Churchill alisisitiza kwamba ili mtu afaulu maishani ni sharti awe na nidhamu.

"Nidhamu hukufikisha mtu mbali na huimarisha uhusiano kazini. Ukiwaheshimu watu kazini, nawe utaheshimiwa vile vile," alisema.

Churchil alihojiwa katika kikao kilichoandaliwa ili kutunuku watumizi wa YouTube ambao wamefikia malengo fulani.

Alitunukiwa Golden Button Award kwa kufikia watumizi zaidi ya milioni moja katika YouTube, Oktoba 30.