Mcheshi Idris Sultan ajipata taabani kwa kumkejeli Magufuli

idris sultan
idris sultan

Msanii maarufu nchini Tanzania ameambiwa ajisalimishe polisi baada ya kuweka picha yake katika mtandao wa kijamii huku picha hiyo ikiwa na sura ya rais Magufuli.

Mchekeshaji huyo ambaye aliwahi kuwa mshindi wa kipindi cha televisheni cha uhalisia cha 'Big Brother Africa' Idris Sultan.

Picha hizo mbili zinaonyesha kichwa cha Magufuli katika kiwiliwili huku picha moja akiwa amevaa suti huku amekaa kwenye kiti cha rais na nyingine akiwa amesimama huku amevaa mtindo wa 'suspender'.

Huku picha hizo zikiwa zinasindikizwa na ujumbe kuwa "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani".

Siku ya Jumanne,rais Magufuli alikuwa anasheherekea miaka 60 ya kuzaliwa, sherehe ambayo wananchi wa taifa hilo walitumia mitandao ya kijamii kwa wingi kutuma salamu zao kwa rais.

Siku hiyo rais alipewa hata majina mapya labda hakuwahi kuyasikia kabla, wengine walimuita 'Mzee baba' wengine 'Jembe' na kusheheni sifa kadhaa katika vituo vya radio na televisheni.

Lakini utani dhidi ya rais uliingia ukakasi pale ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, alipotoa amri kuwa Sultan anapaswa akamatwe na polisi.

Makonda alichangia katika mtandao wa kijamii na kumtaka mchekeshaji huyo kwenda polisi.

"Naona mipaka ya kazi yako huijui, nenda sasa hivi kituo chochote cha polisi uwaambie Makonda kaniambia nije utakuta ujumbe wako," Makonda alisema.

https://www.instagram.com/p/B4PJ8FPHVbo/?utm_source=ig_embed

Wakati huohuo waziri wa Maliasili na Utalii nchini humo Dkt. Hamisi Kigwangalla aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akisema kuwa, "nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi."

Aliongeza kwa kuandika kwenye kurasa yake ya twitter kuwa yuko tayari kumuwekea dhamana mchekeshaji huyo.

Inawezekana Sultan akahukumiwa kwa kosa la kosa la uharifu mtandaoni , sheria ambayo imekuwa ikipingwa na wanaharakati wengi nchini humo.

Hata hivyo hiki kinachotokea Tanzania sasa kwa msanii kushakiwa kwa kujeli kiongozi wa nchi au familia ya kiongozi.

-BBC