Mchujo wa chama ODM ushaanza tayari. Fahamu wagombeaji na sheria za zoezi

Zoezi la mchujo wa chama cha ODM limeanza na kwa sasa linaendelea huku wagombea 10 wakitafuta tikiti ya chama hiki katika eneo bunge la Kibra. Wagombeaji hawa ni Stephen Okello Oguwa, Christone Odhiambo Awino, Peter Ochieng Orero, Tony Ogola Sira Sine, Reuben William Ayako Ojijo, Obaricks Eric Ochieng Obayi, Brian Shem Owino, Benson Musungu, John Milla Otieno na Bernard Otieno Okoth.

Soma mengine hapa:

Vituo vya kupiga kura vilikuwa mlango wazi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi na zinatarajiwa kufungwa saa kumi na moja jioni. Bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya chama cha ODM imetoa taarifa kuwa kura zitahesabiwa katika vituo vya kupigia kura na hatimaye zitatumwa katika katika kituo cha kuhesabu. Katika kituo hicho cha kuhesabu tangazo la mshindi litasubiriwa.

Soma mengine hapa:

 ODM ilitangaza kuwa zoezi hilo litakuwa la wazi na la kuaminika huku ikiwataka wananchi wadumishe amani na utulivu

Mgombeaji yeyote yule atakayekiuka kanuni za zoezi hili la uteuzi na kujihusisha katika kuvuruga na kutofuata sheria za uchaguzi atatemwa nje. Wagombeaji wanaombwa pia wasonge mbali na vituo vya kupiga kura baada ya kupiga kura.

Soma mengine hapa:

Atakayeongoza katika mchujo huu atamenyana na farasi wa Jubilee Macdonald Marigana Eliud Owalo wa ANC.