Mfanyi Biashara Ashtakiwa Kwa Madai Kuwanajisi Watoto Watatu

3
3
Mfanyibiashara mmoja ameshtakiwa kwa uwanajisi watoto watatu.  Mwanamume  huyo wa umri wa miaka  50 kwa jina Albert Nchabera Ongera anadaiwa kuwatendea unyama watoto hao wa umri wa kati ya miaka 8 na 10 manmo Februari mwaka huu.

Hata hivyo amekana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1.5 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Francis Andayi dhamana ya pesa taslim haiwezi kutolewa katika kosa kubwa kama hilo. Kesi hiyo itaskizwa Julai 13.