Mgogoro mpya kuhusu malipo ya walimu wazuka

Photo source: tuko.co.ke

Matumaini ya walimu kupokea mishahara yao ya mwezi Septemba yamedidimia kufuatia hatua ya tume ya kuwaajiri TSC kwenda mahakamani kupinga kutoa malipo hayo.

Kesi hiyo sasa itasikizwa alhamisi wiki ijayo na kuipelekea TSC kuvunja ahadi iliyotolewa wakati wa mazungumzo kati ya miungano ya walimu na rais Uhuru Kenyatta kwamba kesi zote kuhusu mzozo wa malipo ya walimu ziondolewe kortini.