Mguu Niponye!Madaktari na Wauguzi wa Kakamega watoka mbio baada ya mgonjwa wa daalili za virusi vya Corona kuletwa

corona 2
corona 2
Madaktari na wauguzi katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya   Kaunti ya Kakamega  walitoroka kutoka wadi  moja baada ya mgonjwa aliyekuwa na daalili kama za virusi vya Corona kuletwa .

Wahudumu hao wa afya  walihofia kuambukizwa ugonjwa huo  kwa sababu hakuwa na vifaa vya kutosha kujikinga .

Tukio hilo lilizua hofu katika hospitali hiyo   na  baadaye mwendo wa saa sita mchana msimamizi wa hospitali hiyo alipoagiza kufungwa kwa  Milango yote ya kuingia  kwenye taasisi akisema hakuna mgonjwa mwingine atakayeruhisiwa kuletwa . Mgonjwa huyo baadaye alipelekwa katika wadi iliyotengwa  ndani ya hospitali .