Mhubiri atiwa nguvuni kwa kumbaka msichana, Ol Kalou

Mhubiri mwenye umri wa miaka, 37 wa kanisa la Presbyterian Church of East Africa (PCEA) ametiwa nguvuni kwa kosa la kumnajisi msichana wa miaka 16 katika mtaa wa Site, mjini Ol Kalou.

Mhubiri huyo kwa jina Maina Mwangi alitenda kitendo hicho jana jioni.

Inasemekana Maina alikuwa ameenda kutafuta nyumba ya kukodisha nyumbani kwa shangazi ya msichana huyo ambapo alimpata na binamu yake, na kuomba kuonesha nyumba iliyo wazi (vacant).

Hapo ndipo alipomfumania msichana huyo na kumfunga mdomo na baadaye kumpa vitisho vikali iwapo atasema kilichotokea.

Baada ya kuondoka, mwanadada huyo alimuita shangaziye ambaye alimkimbiza hospitalini.

Mshukiwa ambaye ni mwanafunzi wa somo la kitheolojia katika chuo kikuu cha St. Pauls alikubali mashtaka baada ya wakazi waliojawa na hamaki kumkamata asubuhi ya leo.

Wakazi hao walimpeleka hadi kituo cha polisi cha Ol Kalou.

Kisa hicho kiliwaacha wakazi ambao huhudhuria ibada zake na mshangao mkuu kwani anajulikana na wengi kama mtumishi mkuu wa mungu.

Mwangi ana mke na watoto watatu.

-NDICHU Wainaina