Mhubiri James Ng'ang'a aomba Linus Kaika msamaha hadharani

james ng'ang'a
james ng'ang'a
Mhubiri maarufu James Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelism Centre siku ya Jumatatu alimuomba msamaha mwanahabari wa Citizen Linus Kaikai.

Mhubiri huyo aliomba msamaha mbele ya hakimu mkuu Patricia Gichohi katika korti ya Kiambu baada ya kutishia kumuua Kaikai mwezi Mechi mwaka huu.

"Naomba msamaha wako bwana Kaikai, sikumaanisha hayo..pole kwa hayo." Ng'ang'a alisema.

Kupitia mtandao wa Twitter, Kaikai alikubali msamaha wake Ng'ang'a na kumsamehe.

"Leo nimeamua kumsamehe mhubiri James Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelism kwa vitisho dhidi ya maisha yangu mwezi mechi mwaka huu,"Kaikai alisema.

Ng'ang'a  alishtakiwa kwa kutishia kumuua mwanahabari huyo wa runinga ya Citizen mwezi Mechi.

Ng'ang'a pia alishtakiwa kwa kosa la kuchochea vurugu na pia kukosa kutii sheria. Hakimu huyo aliagizi mhubiri huyo awachiliwe kwa dhamana ya shilingi 200,000.

Hii ilikuwa baada ya Kaikai kulalamika kuwa alihisi ametishiwa kupitia kanda ambayo ilizalishwa na mhubiri huyo akimtusi.

https://twitter.com/LinusKaikai/status/1165909353100132357?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1165909353100132357&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.the-star.co.ke%2Fnews%2F2019-08-26-pastor-nganga-publicly-apologises-to-linus-kaikai%2F