Sadio Mane aongoza kwenye ordha ya washambulizi bora wa msimu

Mshambulizi wa Senegal na Liverpool, Sadio Mane ni miongoni mwa wachezaji waliochaguliwa kuwania tuzo la mshambulizi bora wa msimu barani ulaya msimu uliopita.

Mane anawania tuzo la mshambulizi bora huku wapinzani wake wakiwa ni Lionel Messi wa Barcelona pamoja na Cristiano Ronaldo wa Juventus.

Mane alicheka na wavu mara nne huku akipika magoli mawili pamoja na kuisaidia klabu ya Liverpool kutwaa taji la klabu bingwa barani ulaya.

Messi alifunga magoli kumi na mawili huku akipika mengine matatu ila alishindwa kuifikisha Barcelona kwenye fainali ya Klabu bingwa barani ulaya. Ronaldo naye alicheka na wavu mara sita huku akipika mengine mawili.

Kwenye kitengo cha viungo bora wa msimu, Christian Eriksen wa Totenham Hotspurs atawania tuzo hilo na aliyekuwa kiungo wa Ajax, Frankie De Jong aliyejiunga na Barcelona msimu huu. Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson anakamilisha orodha ya viungo bora.

Virgil Van Dirk anaongoza kwenye orodha ya wakali watakaowania tuzo la mlinzi bora wa msimu ya mwaka 2018/2019. Van Dirk anatawania tuzo hilo pamoja na Matthijs De Ligt wa Juventus pamoja na Alexandre Arnold wa Liverpool.

Mlinda lango wa Liverpool Allison Becker atawania tuzo la mlindalango wa mwaka pamoja na Hugo Lloris wa Totenham Hotspurs. Andre Ter Stergen wa Barcelona pia yumo kwenye orodha ya walindalango bora wa msimu.

Washindi wa tuzo hizo watatangazwa mnamo tarehe 29 mwezi huu wakati wa kufanyika kwa droo ya mechi za makundi za klabu bingwa barani ulaya.