Ethiopia yang'aa katika mashindano ya Berlin Marathon huku Kenya ikinyakua fedha

Muhtasari

•Bethwel Yegon ameibuka wa pili baada ya kukimbia kwa masaa mawili, dakika sita na sekunde 14 na kuwa Mkenya wa kwanza kwenye mashidano hayo.

Image: BERLIN MARATHON 2021

Mwanariadha Guye Adola amemaliza katika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Berlin Marathon ambayo yalifanyika Ujerumani asubuhi ya Jumapili.

Adola amemaliza mbio hizo za umbali wa kilomita 42 na kwa masaa mawili, dakika tano na sekunde 42.

Bethwel Yegon ameibuka wa pili baada ya kukimbia kwa masaa mawili, dakika sita na sekunde 14 na kuwa Mkenya wa kwanza kwenye mashidano hayo.

Nafasi ya tatu imenyakuliwa na Kenenisa Bekele kutoka Ethiopia  ambaye ametumia masaa mawili, dakika sita na sekunde 47 kumaliza mbio hizo.

Wakenya wengine ambao wameshiriki katika mbio hizo ni pamoja na Cosmas Muteti, Philemon Kacheran, Bernard Kimeli na Hosea Kipkemboi  ambao wamemaliza katika nafasi ya 5, 6, 8 na 10 mtawalia.