Nike yamsherehekea Kipchoge kwa kuzindua sanamu yake katika makao yao makuu Marekani

Eliud Kipchoge amewapogeza wadhamini wake kwa kuzidua mchogo wake

Muhtasari

•Kipchoge kupitia kwenye ukurasa wake wa  X, ametoa shukrani zake kwa wafadhili wake kwa heshima hiyo kubwa zaidi kwake

Nike ilizindua sanamu ya Eliud Kipchoge katika makao makuu yake huko Beaverton, Oregon, Marekani
Nike ilizindua sanamu ya Eliud Kipchoge katika makao makuu yake huko Beaverton, Oregon, Marekani

Bingwa wa mbio za marathon Eliud Kipchoge ametambuliwa na mfadhili wake Nike kwa njia ya mbio iliyopewa jina lake katika makao makuu ya Ulaya ya kampuni hiyo nchini Uholanzi.

Nike pia  ilizindua sanamu ya Eliud Kipchoge katika makao makuu yake mjini Beaverton, Oregon, Marekani.

Kipchoge kupitia kwenye ukurasa wake wa  X, ametoa shukrani zake kwa wafadhili wake kwa heshima hiyo kubwa zaidi kwake.

"Nike na mimi tumekuwa washirika katika kukimbia  tangu 2003, Nike imekuwa na jukumu muhimu katika kazi yangu, kutoa msukumo na uvumbuzi," alisema kwenye mtandao wake.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 38  alipongeza kampuni hiyo akisema, "asante Nike kwa ushirikiano mzuri, kwa pamoja tunaendesha mbio hizi kama kitu kimoja,"

Tangu aliposhirikiana na Nike, Kipchoge ameweka rekodi kubwa katika maisha yake tangu kushinda mataji mawili ya Olimpiki katika mbio za marathon hadi kuwa mwanariadha wa kwanza katika historia kushinda Berlin Marathon mara tano.

Zaidi ya hayo, akawa mwanamume wa kwanza kukimbia mbio za marathon kwa chini ya saa mbili Tarehe 12 Oktoba 2019 huko Vienna, Austria katika mbio zisizo rasmi zinazoitwa Ineos 1:59 Challenge.

Kipchoge pia ni bingwa mara nne wa London Marathon,Pia alifanikiwa kuvunja rekodi ya dunia ya marathon mara mbili.