Mwanariadha marehemu Kelvin Kiptum ashinda tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2023

Kiptum ambaye alipoteza maisha yake katika ajali ya barabarani Februari 11 anakuwa mtu wa kwanza katika historia ya tuzo za SOYA kupokezwa tuzo angali amekufa.

Muhtasari

• Tuzo ya marehemu Kiptum ilichukuliwa na Patrick Makau ambaye alielekea kwenye ukumbi akiwa na hisia nyingi.

Kelvin Kiptum
Kelvin Kiptum
Image: HISANI

Wiki chache baada ya kuzikwa, mwanariadha wa mbio za masafa marefu, Kelvin Kiptum ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo za SOYA usiku wa kumakia Jumamosi Machi 2.

Hafla ya kutolewa kwa tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa KICC.

Kiptum alishinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume kwa mwaka 2023 huku Faith Kipyegon akishinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kike.

Tuzo ya marehemu Kiptum ilichukuliwa na Patrick Makau ambaye alielekea kwenye ukumbi akiwa na hisia nyingi.

Kwa upande mwingine, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa mpigo kwa Kipyegon kushinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kike, kufuatia msururu bora wa mbio katika miaka ya hivi karibuni.

Kiptum ambaye alipoteza maisha yake katika ajali ya barabarani Februari 11 pamoja na mkufunzi wake kutokea Rwanda anakuwa mtu wa kwanza katika historia ya tuzo za SOYA kupokezwa tuzo angali amekufa.

Wakati huo huo, tuzo za SOYA zilikuwa zinaadhimisha miaka 20 tangu uzinduzi wao na mwanzilishi Paul Tergat, ambaye ni mwanariadha mstaafu.