Conjestina arejea kucheza ndondi baada ya kuugua kutokuwa sawa kwa muda mrefu

Conjestina alikuwa ameacha kushiriki mchezo wa ngumi baada ya kuugua matatizo ya kiakili.

Muhtasari

• Pigano hilo dhidi ya gwiji mwenzake kwenye ulingo huo wa ndondi Fautuma Zarika, liliandaliwa na gavana wa zamani Mike Sonko.

• Pigano hilo aidha liliisha sare, hakuna kati yao aliyeibuka mshindi.

Bondia Conjestina Achieng na Fatuma Zarika.
Bondia Conjestina Achieng na Fatuma Zarika.
Image: TWITTER/MIKE SONKO

Mwanabondia Conjestina Ochieng amerejea uwanjani baada ya kupokea matibabu kwa muda sasa kwenye kituo cha kurekebisha hali ya Mombasa Women Empowerment Network.

Pigano hilo dhidi ya gwiji mwenzake kwenye ulingo huo wa ndondi Fautuma Zarika, liliandaliwa na gavana wa zamani Mike Sonko.

Sonko ambaye alimuokoa Mwanabondia huyo kutoka kijiji chao katika kaunti ya siaya baada ya lejendari huyo kuugua matatizo ya kiakili.

Pigano hilo aidha liliisha sare, hakuna kati yao aliyeibuka mshindi.

Kulingana na Mike Sonko lengo kuu la pigano hilo ilikuwa ni kumrudisha Conjestina kwenye ndondi baada ya kupata matibabu.

"Hadithi ya Conje ni moja ya matumaini ya mpiganaji ambayo inakataa kuzimwa. Licha ya kukabiliwa na changamoto na vikwazo maishani, amerejea akiwa na nguvu na dhamira kuliko hapo awali. Katika safari yake yote ya matibabu, Conjestina ameonyesha nguvu za ajabu kimwili na kiakili.kutaka kwake kujiboresha imewatia moyo vijana wengi ambao walikuwa karibu kukata tamaa maishani,"  Sonko alisema.

Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa kati duniani amekuwa akiuugua kwa muda sasa na kupelekwa hopitalini mara kathaa bila kupata nafuu, hadi ikamlazimu gavana wa zamani wa Nairobi, Mike Sonko, kumhamisha kutoka nyumbani kwake Siaya hadi Mombasa.

Baada ya miezi 11 ya kuokolewa na mike Sonko, hatimaye Conjestina ameonyesha ishara za kupata nafuu na kurejea kwa ndondi.

Mike Sonko pia alihakikishia wanahabari na Wakenya kuwa atamfadhili Conjestina kurejea uwanjani na hatakubali mwanabondia huyo kurudi Siaya.