•Michuano hiyo ilifaa kuchezwa mwaka jana ila ikaahirishwa hadi mwaka huu kutokana na mlipuko wa homa ya COVID 19
•Kundi la kuangaziwa sana ni kundi la F ambalo lina wachezaji matata wakiwemo Christiano Ronaldo, Kieran Mbappe, Manuel Nuer na wengine
Hatimaye michuano ya EURO 2020 iliyokuwa imesubiriwa sana inatarajiwa kuanza usiku wa Ijumaa, Juni 11.
Michuano hiyo ambayo ilifaa kuchezwa mwaka jana ila ikaahirishwa hadi mwaka huu kutokana na mlipuko wa homa ya COVID 19 unatarajiwa kuanza na mechi kati ya Uturuki na Italia itakayochezwa saa nne usiku, masaa ya Afrika Mashariki.
Jumla ya mataifa 24 ya Bara Ulaya yameshirikishwa kwenye Kombe hilo linalotarajiwa kuchezwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Mataifa yanayoangaziwa sana ni pamoja na mabingwa wa kombe hilo mwaka wa 2016 Ureno, Uingereza, mabingwa wa Kombe la dunia Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ubelgiji na Uhispania.
Michuano hiyo imegawanyishwa katika makundi sita yenye timu nne kila kikundi. Haya hapa makundi hayo;
Kundi A:Uturuki, Uswisi, Italia, Welisi
Kundi B: Urusi, Ubelgiji, Udenmarki, Ufini
Kundi C: Austria, Uholanzi, Masedonia Kaskazini, Ukreni
Kundi D: Ucheki, Kroatia, Uskoti,, Uingereza
Kundi E: Uswidi, Poland, Uhispania, Slovakia
Kundi F: Ujerumani, Ufaransa, Ureno, Hungaria
Kundi la kuangaziwa sana ni kundi la F ambalo lina wachezaji matata wakiwemo Christiano Ronaldo, Kieran Mbappe, Manuel Nuer na wengine