LIGI KUU UINGEREZA

Chelsea yapatia kocha na wachezaji wawili mkataba mpya

Kocha mkuu Thomas Tuchel ametia saini mkataba mpya hadi mwezi Juni 2024 huku mshambulizi Olivier Giroud na mlinzi matata Thiago Silva wakiongezewa mwaka moja kila mmoja

Muhtasari

•Mkataba wa Giroud na Silva utatamatika mwishoni mwa msimu wa 2021/22.

•Tuchel ambaye alijiunga na klabu ya Chelsea mwishoni mwa mwezi Januari baada ya kutemwa kwa aliyekuwa kocha Frank Lampard amesaidia klabu hiyo ya jiji la London kushinda kombe la mabingwa bara Ulaya.

Thomas Tuchel
Thomas Tuchel
Image: Twitter

Klabu ya Chelsea imetangaza kuongezewa kwa mkataba wa kocha mkuu na wachezaji wawili.

Kocha mkuu Thomas Tuchel ametia saini mkataba mpya ambao utaisha mwezi Juni mwaka wa 2024.

Mshambulizi Olivier Giroud na mlinzi matata Thiago Silva pia wameongezea muda wa mwaka moja kila mmoja wao.

Mkataba wa wawili hao utatamatika mwishoni mwa msimu wa 2021/22.

Tuchel ambaye alijiunga na klabu ya Chelsea mwishoni mwa mwezi Januari baada ya kutemwa kwa aliyekuwa kocha Frank Lampard amesaidia klabu hiyo ya jiji la London kushinda kombe la mabingwa bara Ulaya.

Klabu hiyo pia iliweza kumaliza katika nafasi ya nne kwenye ligi kuu Uingereza na kufika fainali kwenye kombe la FA kabla ya Leicester kukatiza ndoto zao za kuchukua kombe hilo.

Thiago Silva, 36,ambaye alihamia Chelsea kutoka PSG mwanzoni mwa msimu wa 2020/21 amesifiwa na klabu hiyo kwa uzoefu wake.

"Tulipomleta Thiago mwaka jana tulijua kuwa tunaongeza mchezaji wa kimataifa kwenye kikosi. Thiago ameonyeshaa kila mtu Chelsea ubora wake msimu wote na ana ushawishi mkubwa ndani na nje ya uwanja" Mkurugenzi wa klabu hiyo alimsifia Mbrazili huyo.

Olivier Giroud, 34, raia wa Ufaransa aliyejiunga na klabu ya Chelsea kutoka klabu hasidi ya Arsenal mwakani 2018 amefungia klabu hiyo mabao 32 ndani ya kipindi cha miaka tatu na nusu ambayo amechezea klabu hiyo.

Klabu hiyo pia imetangaza kuondoka kwa mlinda lango Willy Caballero baada ya kuchezea klabu hiyo kwa  kipindi cha miaka nne.