Arsenal yanasa saini ya mlinzi Ben White kwa pauni 50M

Arsenal imekuwa ikiwinda mchezaji huyo matata mwenye umri wa ujana kwa muda sasa.

Muhtasari

•Arsenal iltoa tangazo rasmi kuhusu uhamisho huo siku ya Alhamisi baada ya mchezaji huyo kutia saini mkataba wa miaka mitano.

•White alihusishwa katika kikosi cha Uingereza ambacho kilicheza katika michuano ya Euro 2020 na kumaliza wa pili baada ya kupigwa na Italia kwenye fainali.

Kocha Mikel Arteta, Ben White na Edu
Kocha Mikel Arteta, Ben White na Edu
Image: TWITTER// ARSENAL

Mlinzi wa timu ya kitaifa ya Uingereza Ben White atavalia jazi nyekundu msimu ujao baada ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Arsenal kutoka Brighton & Hoves Albion.

Arsenal iltoa tangazo rasmi kuhusu uhamisho huo siku ya Alhamisi baada ya mchezaji huyo kutia saini mkataba wa miaka mitano.

"Ben White amejiunga nasi kutoka Brighton  & Hove Albion kwa kandarasi ya miaka mingi. Mlinzi huyo wa miaka 23 ambaye amejionyesha kuwa mmoja wa wachezaji wadogo wazuri anajiunga nasi baada ya kuhusishwa kwenye kikosi cha Uingereza kilichocheza kwenye Euro" Arsenal ilitangaza kupitia tovuti yake rasmi.

Inafahamika kuwa White, 23, aligharimu Arsenal pauni milioni 50 na atavalia jazi nambari 4.

White alihusishwa katika kikosi cha Uingereza ambacho kilicheza katika michuano ya Euro 2020 na kumaliza wa pili baada ya kupigwa na Italia kwenye fainali.

Arsenal imekuwa ikiwinda mchezaji huyo matata mwenye umri wa ujana kwa muda sasa.

White alisema kuwa alifurahia sana kujiunga na klabu hiyo ya London.

"Imechukua muda kuliko nilivyotarajia ila nafurahia kuwa hapa sasa" White alisema.