Newcastle yasajili Eddie Howe kama kocha mkuu

Muhtasari

•Kocha huyo wa zamani wa Bournemouth  mwenye umri wa miaka 43  alisajiliwa siku ya Jumatatu kujaza nafasi iliyowachwa wazo na Steve Bruce takriban wiki tatu zilizopita.

•Ametia saini kandarasi ya miaka mitatu na klabu hiyo ambayo kwa sasa iko katika nafasi ya 19 huku ikiwa imenyakua pointi 5 pekee katika mechi 11 ambazo zimechezwa tayari.

Eddie Howe
Eddie Howe
Image: HISANI

Klabu ya Newcastle United imemsajili Eddie Howe kama kocha wake mpya.

Kocha huyo wa zamani wa Bournemouth  mwenye umri wa miaka 43  alisajiliwa siku ya Jumatatu kujaza nafasi iliyowachwa wazo na Steve Bruce takriban wiki tatu zilizopita.

Howe amesema ameridhishwa na nafasi aliyopewa huku akiahidi kutia bidii uwanjani ili kutoa Newcastle katika nafasi mbaya ambayo imekalia sasa kwenye jedwali.

"Hii ni nafasi nzuri lakini kuna kazi kubwa mbele yetu. Hata hivyo nina hamu kubwa ya kuingia uwanjani na kuanza kazi na wachezaji" Howe alisema wakati wa usajili huo.

Raia huyo wa Uingereza ametia saini kandarasi ya miaka mitatu na klabu hiyo ambayo kwa sasa iko katika nafasi ya 19 huku ikiwa imenyakua pointi 5 pekee katika mechi 11 ambazo zimechezwa tayari.

Hatua hii inajiri wiki chache tu baada ya Newcastle kumtimua kazini kocha Steve Bruce kufuatia msururu wa matokeo mabaya.

Bruce ambaye ana umri wa miaka 60 aliondoka Newcastle baada ya kuhudumu  kwa kipindi cha takriban miaka miwili.

Kabla ya kufutwa kwa Bruce klabu hiyo ilipata wamiliki wapya kutoka Saudia wanaoaminika kuwa mabwenyenye wakubwa kweli.