Mohamed Salah: Mshambuliaji wa Liverpool anakaribia kuweka rekodi nyingine ya EPL

Muhtasari

•Rekodi kuu inaweza kuwa ni ya mfungaji bora zaidi wa magoli wa Liverpool katika EPL.

Image: GETTY IMAGES

"Ni wa ajabu.Kusema kweli, hivi sasa, ni mchezaji bora duniani ."

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anaweza kuwa mwenye upendeleo, lakini amekuwa na katika fursa bora ya kushuhudia kuimarika na ukomavu wa soka wa mshambuliaji Mohamed Salah – na mchezaji wa kimataifa wa Misri ambaye anaweza kushikilia rekodi nyingine hivi karibuni.

Salah mwenye umri wa miaka 29 alifunga au kusaidia kufungwa kwa magoli katika mechi ya Jumatatu iliyochezwa nyumbani dhidi ya New Castle iliyowekwa katika nafasi ya 19.

Image: GETTY IMAGES

Mbali na hayo Mo hakuwahi kushindwa kushinda dhidi ya Anfield – halafu Salaha alisawazisha rekodi ya Jamie Vardy ya kufunga mabao au kusababisha bao katika mechi 15 mfulirizo za Primia Ligi.

Lakini suala la kuweka rekodi sio kitu kipya kwa Salah.

Rekodi ya magoli kwa mechi 100 za Primia Ligi
Rekodi ya magoli kwa mechi 100 za Primia Ligi
Image: GETTY IMAGES

Lakini je, ni rekodi gani anayoweza kuipata Salah katika kipindi kilichosalia cha msimu huu ?

Rekodi kuu inaweza kuwa ni ya mfungaji bora zaidi wa magoli wa Liverpool katika Pirimia ligi.

Robbie Fowler (aliyefunga mabao 128 ya ligi katika mechi 266 kwa ajili ya Reds) ndiye anayeshikilia rekodi hii kwa sasa, akifuatiwa na Steven Gerrard (mabao 120 , mechi 504 ), Michael Owen (magoli 118 , mechi 216 ) na Salah (magoli 109 )