Pigo kwa Arsenal baada ya kocha Mikel Arteta kupatikana na Covid-19

Muhtasari

•Arteta ameisimamia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili sasa atakosekana katika mechi kubwa ijayo dhidi ya Manchester City ambayo itachezwa Jumamosi.

Mikel Arteta wa Arsenal
Mikel Arteta wa Arsenal
Image: GETTY IMAGES

Klabu ya Arsenal inazikosa huduma za kocha mkuu Mikel Arteta baada yake kupimwa na kupatikana na virusi vya Corona.

Arsenal imethibitisha kuugua kwa Mhispania huyo kupitia tovuti rasmi ya klabu huku ikieleza kuwa  kwa sasa amejitenga.

Pigo kwa Arsenal baada ya kocha Mikel Arteta kupatikana na Covid-19

"Mikel Arteta atakosa mechi yetu dhidi ya Manchester City Siku ya Mwaka Mpya baada ya kupatikana na COVID-19. Mikel anajitenga kulingana na miongozo ya Serikali na tunamtakia heri" Arsenal imetangaza.

Wanabunduki ambao kwa sasa wamekalia nafasi ya nne na pointi 47 watamenyana na mabingwa watetezi wa EPL Manchester City  Jumamosi mwendo wa saa tisa unusu ugani Emirates.

Mechi yao dhidi ya Wolves iliyotarajiwa kuchezwa Jumanne usiku iliaahirishwa kufuatia ombi lililowasilishwa na timu hiyo ya Bruno Lage.