Maajabu! refa atamatisha mechi kabla ya dakika 90 - AFCON

Muhtasari

• Janny Sikwaze alipuliza kipenga cha mwisho mapema mara mbili wakati wa mechi ya Kombe la Mataifa la  Afrika(AFCON)  2021 katika mechi ya  Tunisia na Mali.

Janny Sikwaze
Janny Sikwaze
Image: hisani

Refa raia wa Zambia Janny Sikwaze alipuliza kipenga cha mwisho mapema mara mbili wakati wa mechi ya Kombe la Taifa Bingwa Barani Afrika ka(AFCON)  2021 katika mechi ya  Tunisis na Mali.

Mwamuzi huyo alimaliza mechi hio, dakika 89 na sekunde 49.

Wakufunzi wa Tunisia walilamika baada ya mechi kufikia tamati wakihoji maamuzi ya kutilia shaka ya refa kumaliza mchezo mapema mara mbili mwanzo katika dakika ya 85 kabla ya kuagiza iendelee na kisha kuimaliza kabisa katika dakika 89.

Alizingirwa na wachezaji wa pande zote mbili  na kuhimizwa kuendeleza mechi hio.

Sikwazwe alimpa kiungo wa Mali, El Bilal Toure kadi nyekundu kwa mchezo usio na hatia mnamo dakika ya 87.Wachezaji waliomba atathmini VAR ikiwa mchezaji huyo alicheza visivyo lakini hata baada ya utathmini alishikilia uamuzi huo.

Katika mechi hiyo penalti mbili zilitolewa ambapo Mali walifunga mkwaju wao wa penati huku Tunisia wakipoteza penalti waliopewa. Firimbi ya mwisho ilipulizwa na Mali ikaibuka na ushindi wa bao 1-0.

Sikwazwe ni mwamuzi mwenye uzoefu wa miaka mingi kwani mwaka 2017 alichezesha fainali ya AFCON baina ya Cameroon na Misri, vile vile alisimamia fainali ya Kombe la Dunia la 2016.