Juma lokole apasua mbarika kuhusu aliyekuwa mpenzi wa Harmonize

Muhtasari

• Juma Lokole amejitokeza wazi na kutetea Salam baada ya kuonekana na mpenzi wa zamani wa Harmonize, Sarah  kwenye eneo la Burudani.

• Alikanusha madai kwamba Salam na Sarah wako kwenye mahusiano huku akisema aliyeanzisha mazungumzo alikuwa  Sarah wala si Salam kama watu wanavyosema.

Juma Lokole
Image: Hisani

Mwandani wa Diamond,Juma Lokole amejitokeza wazi na kutetea Salam baada ya kuonekana na mpenzi wa zamani wa Harmonize, Sarah  kwenye eneo la Burudani.

Hivi majuzi kumekuwa na habari zikienea hasa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Sarah amekuwa katika mahusiano ya siri na mmoja  wa wanachama wa  lebo ya Wasafi.

Lokole kupitia kipindi kimoja  nchini   Tanzania alikanusha madai kwamba Salam na Sarah wako kwenye mahusiano huku akisema aliyeanzisha mazungumzo alikuwa  Sarah wala si Salam kama watu wanavyosema.

"kwanza  acha  niliweke jambo hili kuhusu Salam na  Sarah, wale walikutana Zanzibar...Salam alikuwa kwenye mambo yake ya kukaribisha mwaka mpya  na Sarah alikuwa kwenye mambo yake tunajua alikuja Tanzania na tulimuona juzi aliposti, walikutana si kwa ubaya lakini walikuwa  hawaongei...Sarah  ndiye alimsalimu wa kwanza Salim. Huwa anamuita meneja... kama walitembea pamoja basi.. .walitembea pamoja kwa sababu ya akili ya pombe' alisema Juma Lokole."

Aliendelea kusema sababu ya  mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize kurejea nchini Tanzania ili kufuatilia mali zake.