Kwa miaka yote nilicheza Uingereza, nilihisi upendo wa Malkia - Ronaldo

Ronadlo alisema awali alicheza miaka saba na huu ndio msimu wake wa nane Uingereza.

Muhtasari

• “Ninalipa heshima yangu kwa kumbukumbu yake na ninaomboleza msiba huu usioweza kubadilishwa" - Ronaldo

Ronaldo amemuomboleza malkia Elizabeth
Ronaldo amemuomboleza malkia Elizabeth
Image: Instagram

Mwanasoka maarufu zaidi duniani kwenye mtandao wa Instagram, Mreno Christiano Ronaldo amekuwa mtu wa hivi punde kumuomboleza malkia wa Uingereza, Elizabeth wa paliteaga dunia usiku wa Alhamis.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Christiano alimtaja malkia Elizabeth wa pili kama mtu ambaye hatoweza kusahaulika katika historia ya soka na haswa katika maisha akianza kukipiga kwenye ligi kuu ya Uingereza EPL miaka ya mapema 2000.

Ronaldo alikumbuka alipojiunga kwenye Klabu ya Manchester United akiwa kinda jinsi alivyohisi mazingira ya Uingereza yote yalikuwa yamehanikiza upendo wa watu wake kwa maalkia wao na jambo hilo lilimfanya pia kupenda jinsi malkia alivyokuwaanaenziwa kutokana na uongozi wake weney mfano wa kudumu.

“Miaka saba ya maisha yangu ya uchezaji ilichezwa katika Ligi ya Premia, na kufanya huu kuwa msimu wangu wa 8 kuishi Uingereza. Kwa miaka hii yote, nimehisi upendo wa milele wa Uingereza kwa Malkia, na jinsi Ukuu wake ulivyokuwa muhimu na utakuwa milele kwa watu wa Uingereza,” Ronaldo aliandika.

Mchezaji huo ambaye ni binadamu mwenye ufuatiliaji mkubwa wa umati kwenye mtandao wa Instagram alimuomboleza na kutoa rambirambi zake kwa kusema kwamba kumpoteza malkia Elizabeth wa pili ni pengo ambalo halitakuja kuzibika kabisa kwa miaka na mikaka.

“Ninalipa heshima yangu kwa kumbukumbu yake na ninaomboleza msiba huu usioweza kubadilishwa na nchi ambayo nimejifunza kuiita nyumbani. Mawazo yangu na maombi ni pamoja na Familia ya Kifalme,” Mreno Ronaldo aliandika.

Kufuatia kifo cha malkia huyo mwenye umri wa miaka 96, jana bodi inayosimamia ligi ya premia nchini Uingereza ilikutana na kwa pamoja kuafikiana kuahirisha ligi hiyo mpaka pale malkia atakapozikwa kama njia moja ya kumuenzi na kutoa heshima za mwisho kwa msiba wake.

Awali, Uingereza ilitangaza siku kumi na mbili za maombolezi katika taifa hilo huku shughuli zote muhimu za kuwakusanya watu pamoja ikiwemo michezo, Sanaa na siasa zikisitishwa katika kipindi hicho cha siku kumi na mbili za maombolezi.