Sancho na Pogba watajwa kama wachezaji waliozua matatizo timuni Man Utd kila mara

Matic alisema klabuni Chelsea wachezaji wote walikuwa na nidhamu ya hali ya juu lakini Man Utd baadhi ya wachezaji walikuwa wazembe na wenye kiburi, Sancho na Pogba wakiwa miongoni mwao.

Muhtasari

• Mchezaji wa kimataifa wa Serbia mwenye michezo 48, alicheza mara 189 kwenye kikosi cha United.

• Miezi 18 tu tangu kuondoka kwake na alifichua kwamba Pogba na Sancho walikuwa wazembe wawili.

Sancho na Pogba
Sancho na Pogba
Image: X

Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Nemanja Matic amewataja Paul Pogba na Jadon Sancho kutoka siku zake za Old Trafford kama wachezaji ambao waliendelea kukasirisha kikosi kila mara kwa mienendo yao mibovu timuni.

Matic alisema kwamba wawili hao walikuwa wanachelewa mara kwa mara kuhudhuria mazoezi, jambo ambalo lilikuwa linamuudhi kila mtu katika timu hiyo.

Kiungo huyo wa kati wa Serbia alicheza mechi nyingi zaidi kwa Mashetani Wekundu baada ya kuwasili kwa dili la thamani ya £40m mwaka 2017 wakati wa ukufunzi wa José Mourinho - meneja ambaye alirudi kucheza chini yake katika AS Roma.

Mchezaji wa kimataifa wa Serbia mwenye michezo 48, alicheza mara 189 kwenye kikosi cha United cha kutunga na kupachika mabao manne na asisti 11 katika mlolongo huo akiwa mmoja wa wachezaji bora zaidi.

Alisema kwamba kinyume na Chelsea ambako wachezaji wote walikuwa wenye nidhamu ya hali ya juu, katika timu ya Manchester United baadhi ya wachezaji walikuwa wazembe na wenye kiburi, Sancho na Pogba wakiwa baadhi ya wale aliowataja.

"Huko Chelsea, wachezaji walifanya kazi kwa ustadi, walifika kwa wakati na hawakuwahi kuchelewa mazoezini, lakini kwa United, ilifanyika karibu kila siku. Miongoni mwa wachezaji ambao wangechelewa siku zote ni Paul Pogba na Jadon Sancho na wachezaji wengine kadhaa."

Miezi 18 tu tangu kuondoka kwake na alifichua kwamba Pogba na Sancho walikuwa wazembe wawili ambao mara nyingi wangefika kwenye uwanja wa mazoezi wakiwa wamechelewa, jambo ambalo lilieneza kero kwa wachezaji wenzao.

Katika mahojiano na YU Planet, mchezaji huyo wa zamani wa Roma anadai kwamba alichukua mambo mikononi mwake na alikuwa kiongozi wa 'kamati ya nidhamu ya ndani' wakati wa kukaa kwake kwa misimu mitano Old Trafford huku akijaribu kuondoa viwango vyake kutoka uwanjani.