Gabriel Magalhães na Declan Rice watupiana cheche hadharani Arsenal ikipigwa na Fulham

Baada ya kufungwa bao la 2, wachezaji hao wawili wa Arsenal walionekana kutupiana lawama, Gabriel akimnyooshea Rice kidole cha lawama kwa kutokuwa makini katika mchezo kupelekea bao hilo.

Muhtasari

• Kunako kipindi cha pili, wenyeji Fulham walidhibiti mchezo na kufunga bao la pili na la ushindi.

Rice na Gabriel wkitupiana maneno.
Rice na Gabriel wkitupiana maneno.
Image: x

Wachezaji wa Arsenal, beki Gabriel Magalhães na mchezaji wa kiungo cha kati Declan Rice walionekana wakirushiana cheche kali hadharani pindi tu baada ya Fulham kufunga bao la kusawazisha mchezo kunako Jumapili ya mwisho ya mwaka 2023.

Kuelekea mchezo huo The Gunners walipata nafasi nzuri ya kurejea kileleni mwa jedwali la Premier League, huku wapinzani wao Liverpool na Manchester City wakiwa wamecheza mechi moja pungufu.

Na wanaonekana wako tayari kufanya hivyo tu Bukayo Saka alikuwa mahali pazuri kwa wakati ufaao kugonga mpira uliorudi nyuma na kuwapa The Gunners bao la kuongoza baada ya dakika tano pekee uwanjani Craven Cottage.

Licha ya kwenda nyuma ya kikosi cha Marco Silva walijibu vyema katika kipindi cha kwanza na Raul Jimenez akaunganisha krosi ya Tom Cairney kusawazisha wenyeji kabla ya muda.

Baada ya bao hilo, wachezaji hao wawili wa Arsenal walionekana kutupiana lawama, Gabriel akimnyooshea Rice kidole cha lawama kwa kutokuwa makini katika mchezo kupelekea bao hilo.

Huku udhibiti wa mchezo ukiendelea kutoka kwa wageni baada ya mwendo mgumu wa kufadhaika kulionekana wazi miongoni mwa vijana wa Mikel Arteta uwanjani.

Kunako kipindi cha pili, wenyeji Fulham walidhibiti mchezo na kufunga bao la pili na la ushindi hivyo kuinyima Arsenal nafasi ya kumaliza mwaka wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya premia.

Hiki kilikuwa kichapo cha kwanza kabisa cha Arsenal mikononi mwa Fulham tangu mwaka 2012.

Itakumbukwa wiki iliyopita katika usiku wa kuelekea Krismasi, Arsenal walikuwa kakika nafasi ya kwanza lakini wiki moja baadae, wamemaliza mwaka wakiwa katika nafasi ya nne.