Babake Neymar kumlipia Dani Alves dhamana baada ya kuhukumiwa miaka 4½ jela

Akaunti za Dani Alves zilipigwa tanji katika mchakato wa mahakama na ilionekana kuwa haiwezekani beki huyo wa pembeni kulipa dhamana hiyo kutoka mfukoni mwake.

Muhtasari

• Babake Neymar tayari ametumia hila hii ya kulipa euro 150,000 kama fidia kwa mwathiriwa aliyeathiriwa na uhalifu wake wa unyanyasaji wa kijinsia., jarida hilo lilisema.

Dani Alves
Image: BBC

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil na timu ya klabu ya Barcelona, Dani Alves anatazamiwa kuachiliwa kutoka jela akisubiri rufaa dhidi ya hukumu yake ya ubakaji.

Alves ataka kuachiliwa kwa dhamana euro milioni moja ($1.08 milioni), mahakama ya Barcelona ilisema Jumatano.

Uamuzi huo ulikuja siku moja baada ya wakili wake kuomba kuachiliwa kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa misingi kuwa tayari alikuwa ametumikia robo ya kifungo chake cha miaka minne na nusu katika kizuizi cha kabla ya kesi yake kukamatwa Januari 2023.

Akaunti za Dani Alves zilipigwa tanji katika mchakato wa mahakama na ilionekana kuwa haiwezekani beki huyo wa pembeni kulipa dhamana hiyo kutoka mfukoni mwake, lakini kwa mujibu wa Fabrizio Romano na jarida la  'La Vanguardia', babake Neymar ndiye atakayekuwa na jukumu la kuweka amana dhamana ya euro milioni moja ili mwanasoka huyo wa zamani aachiliwe kutoka jela.

Babake Neymar tayari ametumia hila hii ya kulipa euro 150,000 kama fidia kwa mwathiriwa aliyeathiriwa na uhalifu wake wa unyanyasaji wa kijinsia. Mara babake Neymar atakapoweka dhamana na amri mpya kutolewa ya kuidhinisha, Dani Alves ataachiliwa kwa dhamana.

Alves alihukumiwa tarehe 22 Februari kwa kumbaka mwanamke katika klabu ya usiku ya Sutton huko Barcelona. Matukio hayo yalifanyika mkesha wa Mwaka Mpya 2022 na mchezaji huyo alikamatwa tarehe 20 Januari 2023 baada ya kuitwa kutoa ushahidi.

Tangu wakati huo amebaki gerezani, hivyo tayari amekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja, ambao utaondolewa kwenye kifungo chake mara tu atakapoachiliwa.