Mchambuzi afutwa kazi runingani kwa 'utani' wa ubaguzi wa rangi dhidi ya Lamine Yamal

Burgos kisha akasema: "Ikiwa hatafanya vizuri, anaishia kwenye taa", kisingizio kikiwa kwamba angekuwa maskini kama si soka. Yamal alizaliwa nchini Uhispania na wazazi wa Morocco na Equatorial Guinea.

Muhtasari

• Yamal alizaliwa nchini Uhispania na wazazi wa Morocco na Equatorial Guinea.

• Wachezaji wa Barca na PSG wakikataa kuzungumza na kituo cha televisheni baada ya mechi, baada ya kufahamishwa kuhusu kile kilichosemwa.

• Ricardo Sierra alisema UEFA, Barca na PSG "zilikuwa na hasira sana" kuhusu maoni hayo.

Burgos afutwa kazi kisa kauli ya utani kuhusu Yamal.
Burgos afutwa kazi kisa kauli ya utani kuhusu Yamal.
Image: Hisani

Kituo cha Televisheni cha Uhispania kilimtimua mchambuzi wa spoti German Burgos baada ya 'utani' wa ubaguzi wa rangi uliomlenga nyota wa Barcelona Lamine Yamal.

Yamal, 16, alikuwa mmoja wa nyota wa ushindi wa Barcelona wa 3-2 ugenini dhidi ya Paris Saint-Germain katika mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wiki jana Jumatano usiku.

Lakini matokeo ya timu na uchezaji wake vilifunikwa na maoni yaliyotolewa na Burgos kabla ya kuanza.

Huku kinda huyo wa Barca akionyeshwa akifanya mazoezi ya kupasha misuli moto, mchambuzi mmoja alisema: "Angalia ubora, angalia miguso ya Lamine Yamal."

Kipa wa zamani wa Atletico Madrid na Argentina Burgos kisha akasema: "Ikiwa hatafanya vizuri, anaishia kwenye taa", kisingizio kikiwa kwamba angekuwa maskini kama si soka.

Yamal alizaliwa nchini Uhispania na wazazi wa Morocco na Equatorial Guinea.

Movistar Plus+ ilihisi athari mbaya za maneno ya Burgos mara moja, huku wachezaji wa Barca na PSG wakikataa kuzungumza na kituo cha televisheni baada ya mechi, baada ya kufahamishwa kuhusu kile kilichosemwa.

Ricardo Sierra alisema UEFA, Barca na PSG "zilikuwa na hasira sana" kuhusu maoni hayo.

Burgos, ambaye hapo awali alikuwa meneja msaidizi wa Diego Simeone huko Atleti, aliomba msamaha wa hali ya juu ambapo alisisitiza kwamba maneno yake yalikuwa ya kipuuzi, sio ya kibaguzi, lakini haijamzuia mwajiri wake kumfukuza.

Movistar Plus+ ilisema Alhamisi "watasitisha mara moja makubaliano yao ya ushirikiano" na Burgos na "wangechukua hatua zinazofaa kuhakikisha kuwa matukio kama haya hayajirudii"