Chelsea wanakaribia kumteua Enzo Maresca wa Leicester City kama kocha wao mpya

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 44 aliiongoza Leicester kutwaa ubingwa wa ligi ya Championship msimu uliokamilika na kuwarejesha kwenye EPL, na pia amekuwa kocha msaidizi wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City.

Muhtasari

• Golikipa wa zamani wa Chelsea Caballero anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo kama sehemu ya wafanyakazi wa Maresca.

• Mail Sport wameripoti Maresca anataka kuleta hadi wafanyakazi watano pamoja naye kutoka King Power Stadium.

 

Chelsea wanakaribia kumteua Enzo Maresca wa Leicester City kama meneja anayefuata, huku Muitaliano huyo akitaka kuleta wafanyakazi watano pamoja naye kulingana na ripoti.

The Blues wamefanya harakati za haraka kufuatia kuondoka kwa Mauricio Pochettino Jumanne iliyopita, baada ya kuifundisha kwa msimu mmoja tu Stamford Bridge.

Klabu hiyo inatarajia kukamilisha dili la kumnunua Maresca mwishoni mwa juma, na wanatarajiwa kulipa fidia ya pauni milioni 10 kwa Foxes.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 44 aliiongoza Leicester kutwaa ubingwa wa ligi ya Championship msimu uliokamilika na kuwarejesha kwenye EPL, na pia amekuwa kocha msaidizi wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City.

Wakali hao wa Stamford Bridge wanatazamiwa kumpa Maresca mkataba wa miaka mitano kwa mujibu wa ripoti, huku taarifa za mwisho za mkataba huo zikiwa zimepangwa, pamoja na wafanyakazi ambao Muitaliano huyo anataka kuja naye.

Golikipa wa zamani wa Chelsea Caballero anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo kama sehemu ya wafanyakazi wa Maresca.

Mail Sport wameripoti Maresca anataka kuleta hadi wafanyakazi watano pamoja naye kutoka King Power Stadium.

Jina moja litafahamika kwa mashabiki wa Chelsea na hilo ni golikipa wa zamani Willy Caballero ambaye alikuwa namba mbili wa Maresca katika klabu ya Leicester, huku Mail Sport ikiongeza anatarajiwa kuwa mmoja wa makocha ambao watahama na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 44.

Caballero alikuwa Chelsea kuanzia 2017-2021, baada ya kujiunga kwa uhamisho huru kutoka Manchester City, na aliendelea kucheza mechi 38 akiwa na The Blues.