Makundi ya kufuzu kwa Afcon 2025 yatangazwa; Fahamu Kenya itamenyana na kina nani

Kenya imepangwa katika kundi J la michuano ya kufuzu kwa Afcon 2025.

Muhtasari

•Droo ilifanyika Julai 4, 2024 katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini wakati makundi kumi na mawili yenye timu nne kila moja yalipoundwa.

•Mechi za makundi zitaanza mwezi Septemba 2024 na kumalizika Novemba 2024.

Image: CAF

Kenya imepangwa katika kundi J la michuano ya kufuzu kwa Afcon 2025.

Droo ya makundi ya kufuzu kwa Afcon 2025 ilifanyika Julai 4, 2024 katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini wakati makundi kumi na mawili yenye timu nne kila moja yalipoundwa.

Katika kundi J, Kenya inashiriki pamoja na Cameroon, Namibia na Zimbabwe.

Mechi za makundi zitaanza mwezi Septemba 2024 na kumalizika Novemba 2024 kabla ya mchuano mkuu utakaoanza tarehe 21 Desemba mwaka ujao, na fainali kuchezwa tarehe 18 Januari 2026.

Miamba wa soka kutoka Afrika Kaskazini, Morroco watakuwa wenyeji wa mashindano ya mwaka ujao.

Tazama makundi mbalimbali ya kufuzu Afcon 2025:

Kundi A: Tunisia, Madagascar, Comoro, Gambia

Kundi B: Morocco, Gabon,Jamhuri ya Afrika ya Kati, Lesotho

Kundi C: Misri, Cape Verde, Mauritania, Botswana

Kundi D: Nigeria, Benin Libya, Rwanda

Kundi E: Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia

Kundi F: Ghana, Angola, Sudan, Niger

Kundi G: Cote d'Ivoire, Zambia, Sierra Leone, Chad

Kundi H: DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia

Kundi I: Mali, Msumbiji, Guinea Bissau, Eswatini

Kundi J: Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe

Kundi K: Afrika Kusini, Uganda, Kongo, Sudan Kusini

Kundi L: Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi