“Inatia huruma sana kuona Mbappe aliondoka PSG na kuingia Real bila malipo” – kocha Enrique

"Nilikutana na mchezaji mzuri sana Kylian Mbappe. Mtu wa kiwango cha kipekee. Ni mara chache sana mtu anaweza kukutana na mchezaji wa kiwango chake anapowasili kwenye klabu," Luis Enrique alisema.

Muhtasari

• "Nilikutana na mchezaji mzuri sana Kylian Mbappe. Mtu wa kiwango cha kipekee. Ni mara chache sana mtu anaweza kukutana na mchezaji wa kiwango chake anapowasili kwenye klabu," Luis Enrique.

MBAPPE NA ENRIQUE
MBAPPE NA ENRIQUE
Image: HISANI

Kocha wa PSG ya Ufaransa, Luis Enrique amekiri kwamba ilikuwa huzuni na huruma sana kuona klabu hiyo ikishindwa kumzuia staa wao, Kylian Mbappe kuondoka.

Enrique alisema kwamba ni huruma na aibu kuona staa mkubwa kama Mbappe kuachiliwa kuondoka ugani Par des prince kuenda Real Madrid kwa uhamisho wa bila malipo baada ya mkataba wake kukamilika.

"Nilikutana na mchezaji mzuri sana Kylian Mbappe. Mtu wa kiwango cha kipekee. Ni mara chache sana mtu anaweza kukutana na mchezaji wa kiwango chake anapowasili kwenye klabu," Luis Enrique amesema katika waraka wake wa Movistar.

"Mtu, mwenye mapenzi, karibu... ajabu ya mchezaji. Ni huruma iliyoje ameenda Real Madrid! Hasa kwetu [Paris Saint-Germain] wakati huo," kocha mkuu wa PSG aliongeza.

Kylian Mbappe aliondoka PSG na kwenda Real Madrid kama mchezaji huru msimu uliopita wa joto. Kwa sasa anadai €55m kama mshahara ambao haujalipwa na nyongeza kutoka kwa klabu yake ya zamani.

Mfaransa huyo alicheza mechi 48 chini ya Luis Enrique, akirekodi mchango wa mabao zaidi ya 50.

Shauku ya Enrique kwa Mbappe inaenea zaidi ya uwezo wa mchezaji huyo, akionyesha kuthamini sana sifa zake za kibinafsi.

Ingawa muda wao pamoja PSG ulikuwa mfupi, maneno ya Enrique yanaonyesha jinsi alivyothamini mchango wa nyota huyo wa Ufaransa, kama mchezaji wa soka na kama mtu.

Ingawa PSG wanaweza kupoteza mmoja wa wachezaji bora, Mbappe sasa anaonyesha kipaji chake Real Madrid, huku sifa za kocha wake wa zamani zikiendelea kumfuata.