Mikel Arteta kuondoka Arsenal? Hiki ndicho alichokisema alipoulizwa swali hilo

Ikumbukwe timu hiyo ya Ufaransa imo sokoni kutafuta kocha mpya baada ya kumalizana na kocha wao Christopher Galtier na Arteta amekuwa akihusishwa pakubwa kuhamia huko.

Muhtasari

• Mhispania huyo amefurahia maisha mazuri na Washikaji hao wa London kaskazini tangu kuteuliwa kwake mwaka wa 2019.

Mikel Arteta wa Arsenal
Mikel Arteta wa Arsenal
Image: GETTY IMAGES

Huku joto la uhamisho wa wachezaji likiwa linazidi kupanda katika ligi mbalimbali kote duniani, makocha nao hawajasazwa kwani timu mbalimbali zinatafuta kuboresha vikosi vyao sit u kwa upande wa wachezaji bali pa katika kitengo cha ukufunzi.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda timu mbali mbali za Ulaya, baada ya kufana msimu uliopita ambapo aliongoza Arsenal kumaliza wa pili kwenye ubingwa wa ligi kuu ya EPL, msimu ambao ulitajwa kuwa bora Zaidi kwa timu hiyo kwa Zaidi ya miaka 18.

Hata ivyo, Mkufunzi huyo amefutilia mbali madai ya kuondoka ugani Emirates hivi karibuni, huku kukiwa na uvmi uliokuwa unamhusisha kwenda Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Ikumbukwe timu hiyo ya Ufaransa imo sokoni kutafuta kocha mpya baada ya kumalizana na kocha wao Christopher Galtier.

Mhispania huyo amefurahia maisha mazuri na Washikaji hao wa London kaskazini tangu kuteuliwa kwake mwaka wa 2019.

Arteta aliteuliwa kushika wadhifa huo baada ya kutimuliwa kwa Unai Emery, ambaye alirithi mikoba ya kocha mkuu Arsene Wenger.

Ingawa hakuna uwezekano kwamba nyota huyo wa zamani wa Everton ataitupa Arsenal hivi karibuni, hilo halijazuia tetesi za kumhusisha na majukumu ya PSG.

Kocha mkuu wa zamani wa Barcelona na Uhispania Luis Enrique anaaminika kukaribia kuhamia mji mkuu wa Ufaransa kuchukua nafasi ya Christophe Galtier, ambaye alitimuliwa mapema mwezi huu.

Iwe hivyo, ripoti zimedai kuwa PSG walifanya mazungumzo na Arteta kuhusu uwezekano wa kuhama.

Hata hivyo, nahodha huyo wa zamani wa Arsenal amejitokeza na kuweka wazi kuwa ana furaha katika Uwanja wa Emirates.

 

"Ninaweza kusema tu kwamba nina furaha Arsenal. Ninahisi kupendwa, kuthaminiwa na wamiliki wetu, Stan na Josh [Kroenke], na nina mengi ya kufanya hapa katika klabu hii," aliambia Marca.

"Nina furaha na ninashukuru sana kuwa Arsenal," aliongeza.