Arsenal warejea 'Top 4' kushiriki ligi ya mabingwa ulaya baada ya kiangazi cha miaka 7

Mara ya mwisho kushiriki mashindano hayo 2017, Arsenal waliondolewa Champons League na Bayern kwa kibano cha mabao 10-2 katika hatua ya 16 bora.

Muhtasari

• Kabla ya mwaka huo, Arsenal walikuwa wamefuzu mara 17 mfululizo kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa tangu mwaka 2000.

Arsenal warejea kwenyec ligi ya mabingwa baada ya miaka 7
Arsenal warejea kwenyec ligi ya mabingwa baada ya miaka 7
Image: BBC SPORT

Baada ya miaka saba mirefu ya upweke nje ya mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya, hatimaye timu ya Arsenal imejikatia tikiti ya kurejea kwa kishindo kwenye mashindano hayo yenye hadhi ya nyota tano baada ya kufunga msimu wa 2022/23 katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la ligi kuu ya premia.

Mara ya mwisho kwa Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa msimu wa 2016/17, ikiwa ni kampeni yao ya 17 mfululizo kwenye michuano hiyo na ya saba mfululizo kuondoka katika hatua ya 16 bora.

The Gunners walikuwa wamefuzu baada ya kumaliza kama washindi wa pili katika Ligi ya Premia msimu uliopita na kuongoza kundi lao mbele ya Paris Saint-Germain, Ludogorets Razgrad na Basel, wakishinda nne na kutoka sare mbili kati ya sita walizocheza na kutinga hatua ya mtoano.

Hata hivyo, kilichofuata ni aibu kubwa zaidi katika historia ya klabu hizo, baada ya kuchapwa mabao 5-1, nyumbani na ugenini, na Bayern Munich, na hivyo kuondoka kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 10-2 na mabingwa hao wa Ujerumani.

Katika msimu huo huo, Wenger hakuweza kumaliza katika nafasi nne za juu kwani siku zake za Arsenal zilianza kuhesabika na hivyo kuhitimisha kipindi cha miaka 17 mfululizo ambacho alikuwa amefuzu kwa kikosi cha London kaskazini kwa Ligi ya Mabingwa, iliyoanza mwaka wa 2000/ 01 kampeni.

Msimu huu ulianza kwa nyota ya jaha kwa miamba hao wa ligi ya Uingereza wakati kocha mkuu Mikel Arteta alikwenda kinyume na matarajio ya wengi kwa kuiongoza Arsenal kutoa ushindani mkali kwenye kinyang’anyiro cha Premia, licha ya wengi wa wachezaji wake kuwa wachanga na wasio na uzoefu mkubwa.

Arsenal walishikilia uongozi wa jedwali kwa angalau asilimia 90 ya msimu kabla ya kuja kuutupa uongozi huo muhimu katika mechi 7 za mwisho wa msimu na hivyo kuipa City nafasi ya kulitetea taji hilo kwa mara ya tatu mtawalia.