SOKA KIMATAIFA

Pep Guardiola atajwa kocha bora EPL msimu 2022-2023

Guardiola pia alishinda tuzo hilo katika msimu wa 2017/2018 na 2020/2021

Muhtasari

•Ni mara ya tatu kushinda tuzo la Sir Alex Ferguson baada ya kupigiwa kura na mameneja wote kutoka ligi mbalimbali Uingereza.

•Kocha wa klabu ya Chelsea upande wa kina dada Emma Hayes pia ameshinda taji la Women’s Super League.

Meneja wa Manchester City ametajwa kuwa meneja bora ligi katika ya Uingereza msimu wa 2022/2023 na Shirikisho la Mameneja wa Ligi, LMA.

Guardiola pia alishinda tuzo hilo katika msimu wa 2017/2018 na 2020/2021. Ni mara ya tatu kushinda tuzo la Sir Alex Ferguson baada ya kupigiwa kura na mameneja wote kutoka ligi mbalimbali Uingereza.

Mhispaniola mwenye umri wa miaka 52, pia ameshinda tuzo la kuwa meneja bora katika msimu, aliposhinda ligi kwa mara ya tatu mtawalia na kushinda mara tano kwa misimu sita akiwa Man City.

Kocha wa klabu ya Chelsea upande wa kina dada Emma Hayes pia ameshinda taji la Women’s Super League.

Hili lilikuwa tuzo lake la nne, na sita kwa ujumla.Chini ya Hayes,klabu ya kina dada ya Chelsea imepata taji hilo mara nne, walipoipiku Manchester United kwa alama mbili waliowashinda  na kunyakua taji la FA  kwa mara ya tatu.

Guardiola amekuwa meneja wa tatu kushinda LMA tuzo la meneja bora katika mwaka, kusawazisha idadi ya David Moyes, lakini yupo chini ya Sir Alex Ferguson kwa mataji mawili.

City itakuwa ikichuana na Manchester United Jumamosi katika fainali ya kombe la FA. Ushindi katika mechi hiyo itawapatia nafasi ya  kushinda mataji matatu watakapokuwa wakimenyana na Inter Milan kwenye ligi ya mabingwa Juni 10.

Guardiola alisema; “Ni heshima kubwa sana kupata taji hili. Ni sisi ligi bora zaidi katika ulimwengu na nakuhaidi tutakuwa hapo msimu ujao.”

Lou Macari alishinda tuzo la uzinduzi wa John Dancun Award, linalowakilisha jitihada za kipekee.

Kiungo huyo wa awali wa Manchester United na Celtic amekuwa akiendesha mpango wa kuwapa makao wasio na makao Stoke, ambapo alipata nafasi mbili kama mkufunzi.

Mikel Arteta wa Arsenal, Roberto de Zerbi wa Brighton, Eddie Howe wa Newcastle, Vincent Kompany wa Burnley na Steven Schumacher wa Plymouth ni baadhi ya walioteuliwa katika tuzo hilo.

Kompany na Schumacher wameshinda mataji katika Championship na League One kuwa meneja wa mwaka mtawalia.

Leyton Orient, Meneja Richie Wellens alitetea tuzo la League Two baada ya kushinda ligi.

Katika upande wa ligi ya Championship upande wa kina dada Laureen Smith alishinda taji hilo na Bristol City.