Kayange atambuliwa kama mmoja wa wachezaji bora duniani wa raga wa wakati wote

Muhtasari

•Shirikisho la raga ulimwenguni liliweza kumtambua gwiji huyo mwenye umri wa miaka 39 kama mmoja wa wachezaji bora kot wa wakati wote kote duniani.

•Kayange amehimiza shule na jamii kukumbatia riadha na kusaidia wachezaji wadogo kukuza talanta zao

Image: HISANI

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya raga Humphrey Kayange ametambuliwa kama mmoja wa magwiji wa mchezo huo kote ulimwenguni.

Shirikisho la raga ulimwenguni liliweza kumtambua gwiji huyo mwenye umri wa miaka 39 kama mmoja wa wachezaji bora kot wa wakati wote kote duniani.

Kayange aliorodheshwa pamoja na magwiji wengine kama Osea Kolinesau wa Fiji, Huriana Manuel wa New Zealand, Will Carling wa Uingereza, Jim Telfer wa Uskoti na Cheryl McAfee wa Australia.

Kayange alieleza furaha yake kufuatia hatua hiyo huo huku akiwashukuru wote waliomsaidia kupata mafanikio makubwa kwenye taaluma yake ya kucheza raga.

"Ni jambo la heshima kutambuliwa pamoja na magwiji wengine watano kote ulimwenguni. Nafurahia na kushukuru kwa kutambuliwa, Tuzo hii ni kubwa kunishinda. Inaonyesha usaidizi ambao nimepokea kwa taaluma yangu yote. Nashukuru wachezaji wenzangu, wakufunzi, familia, marafiki, mashabiki na shirika la raga.. ningependa tuzo hii iwe pongezi kwa wote ambao wanacheza, wanafunza raga na kupatia wachezaji wengine motisha" Alisema Kayange.

Kayange amehimiza shule na jamii kukumbatia riadha na kusaidia wachezaji wadogo kukuza talanta zao.